Yanga vs Simba, ugali moto mboga moto

Muktasari:
- Nabi ameshazoea ushindi dhidi ya Simba akiwa na ushindi mara tatu na kutoa sare moja, ataingia katika mchezo huo kutuliza presha ya matokeo kwa timu yake lakini pia akisaka ushindi mwingine wa kumharibia Mgunda katika dabi yake ya kwanza.
KESHO Jumapili kutakuwa na dakika 90 maalum ambazo kila Mtanzania hata kama hupendi mchezo wa soka basi zitahusika kwako japo kwa kusikia kelele za mashabiki wakati klabu kubwa na kongwe mbili Yanga na Simba zitakapokuwa uwanjani pale Kwa Mkapa.
Hii itakuwa mechi ya pili kati ya timu hizo msimu huu lakini ikiwa ya kwanza katika Ligi Kuu Bara, Simba ikitaka kulipa kisasi cha kupoteza dhidi ya watani wao kwa mabao 2-1 katika mchezo wa Ngao ya Jamii.
Kwenye mchezo huo tunakuletea vita ya mtu na mtu kutoka pande zote za timu hizo ambazo kama utazifuatilia utapata burudani nyingine mbali na ile ya vikosi vyote kiujumla.JOASH vs MAYELEBeki wa Simba, Joash Onyango ana uhakika wa kurejea uwanjani kupambana na Yanga lakini safari hii akitaka kuhakikisha hafanyi makosa ya kuruhusu ubabe wa mshambuliaji wa Yanga, Fiston Mayele aliyefunga mabao 13 katika mechi 10.Mara ya mwisho Onyango kuwa uwanjani pale CCM Kirumba katika mchezo kama huu Mayele hakufunga bao lakini pia mshambuliaji huyo amewahi kufumania nyavu mbele ya beki huyo katika mchezo wake wa kwanza wakati anatua Yanga. KISINDA vs TSHABALALAKama Yanga itampa nafasi ya kuanza winga wao Tuisila Kisinda kuna uwezekano mkubwa jamaa akapambana na beki wa kushoto na nahodha msaidizi wa timu hiyo Mohamed Hussein ‘Tshabalala’.Kisi-nda anasifika kwa kasi yake na tukio baya ni pale alipomuacha kwa mbio Onyango kabla ya kuihama timu hiyo, lakini pia Tshabalala ndiye beki ambaye yuko katika kiwango bora kabisa Msimbazi. MWENDA vs MOLOKOBeki wa kulia wa Simba, Israel Mwenda gari linazidi kuchanganya taratibu, akinufaika na majeraha ya mwenzake mkongwe Shomari Kapombe, mchezo huu mtihani wa Mwenda unaweza kuwa kwa winga wa Yanga, Jesus Moloko. DJUMA vs OKRAHBeki wa kulia wa Yanga, Djuma Shaban bado hajaonyesha ubora wake mkubwa kama ambavyo alikuwa AS Vita na katika mchezo huu atakuwa katika vita na winga mwenye kasi na aliye katika kiwango bora wa Simba, Augustine Okrah.Wawili hawa kila mmoja keshafunga bao la frii-kiki katika Ligi Kuu Bara msimu huu. PHIRI vs JOBStaa wa Simba katika kucheka na nyavu ni mshambuliaji Moses Phiri ambaye anaicheza derby yake ya kwanza akiwa na wekundu hao baada ya kuikosa mechi ya Ngao ya Jamii ambayo kocha aliyepita Zoran Maki alimtupa jukwaani.Phiri ni wa moto sana hivi sasa. Amefunga mabao tisa katika mechi tisa alizoitumikia Simba msimu huu, Kasi yake itakuwa ni mtihani mkubwa kwa mabeki wa kati wa Yanga hasa Dickson Job kuhakikisha Mzambia huyo haendelezi saluti zake za kijeshi kila anapofunga bao. CHAMA vs AUCHOKocha wa Simba, Juma Mgunda amekirudisha kiwango cha kiungo fundi Clatous Chama ambaye sasa yuko vizuri kisawasawa na hapa kazi itakuwa kwa viungo wakabaji wa Yanga wakiongozwa na Khalid Aucho.Kama Aucho na wenzake watashindwa kudhibiti kasi ya Chama kuna balaa kubwa litawakuta kutokana na jinsi jamaa alivyo na jicho la kumchungulia Phiri na kumpa pasi muafaka, utakumbuka Chama ndiye aliyetoa asisti ya bao la kuongoza la Simba katika mechi ya Ngao ya Jamii wekundu hao walipolala 2-1. MANULA vs DIARRAKutakuwa na vita nyingine kwa makipa wa timu zote, kipa wa Simba Aishi Manula baada ya kukosa mechi mbili zilizopita dhidi ya Yanga anarudi golini akitambua kwamba timu yake ilipoteza mechi zote mbili huku kipa mwenzake Benno Kakolanya akiruhusu mabao matatu.Manula atataka kuhakikisha mechi hiyo anatoka tena salama kama ilivyokuwa katika mchezo wake wa mwisho dhidi ya Yanga lakini pia mwenzake wa Yanga, Diarra Djigui ambaye alimpokonya tuzo ya kipa bora wa msimu uliopita akitafuta ushindi mwingine kwa wekundu hao akiwa pia hajawahi kupoteza mechi kama hiyo tangu atue Yanga. INONGA vs AZIZI KIBeki wa Simba Henock Inonga atakuwa kazini tena na hapa atakuwa na kazi kubwa ya kuhakikisha kiungo mshambuliaji wa Yanga Stephane Aziz KI anakosa madhara katika mchezo huo.Simba hapa pia inaweza kuwatumia viungo wake wakabaji wakiongozwa na Sadio Kanoute kumtuliza KI ambaye alikuwa na kiwango bora katika mchezo kama huo uliopita. MGUNDA vs NABISimba itakuwa na kocha wao Juma Mgunda na jamaa moto wake umeanza vyema akiwa hajapoteza mchezo wowote tangu atue kwa wekundu hao na sasa anazifikia dakika 90 ambazo kama atashinda atakuwa amesimamisha ufalme wa kocha mwenzake wa Yanga, Nasreddine Nabi.Nabi ameshazoea ushindi dhidi ya Simba akiwa na ushindi mara tatu na kutoa sare moja, ataingia katika mchezo huo kutuliza presha ya matokeo kwa timu yake lakini pia akisaka ushindi mwingine wa kumharibia Mgunda katika dabi yake ya kwanza.