Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga yaibuka na kauli mbiu ya kibabe Wiki ya Mwananchi

Muktasari:

  • Tamasha la Wiki ya Mwananchi linafanyika kwa mara ya sita tangu lilipoanza mwaka 2019.

Yanga imetangaza kuwa Kauli Mbiu yake kwa Tamasha la Wiki ya Mwananchi mwaka 2025 ni ‘Tunapiga Kichwani Tu’.

Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe amesema kuwa Kauli Mbiu hiyo ndio itakayotumika katika msimu wa 2025/2026 ambao itakuwa ikitetea mataji yake ya Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho la CRDB.

“Tamasha hili linabeba fahari yetu, ukubwa wetu, hadhi na thamani yetu kama Dar Young Africans. Tunaomba tiketi zimalizike mapema. 

“Msimu wa 2025/2026 usiwe msimu wa maneno mengi ila uwe msimu wa vitendo. Katika msimu ujao tukakubaliana kwamba kauli mbiu ya msimu huu ni ‘Tunapiga Kichwani Tu’. Hiyo ndio kauli mbiu yetu.

“Msimu huu hatutaki mazoea na watu. Sasa hivi Yanga inapiga kichwani. Ndio tunavyokwenda hivi msimu huu. Sisi tumeshaandaa timu yetu na tumeshatoa nyundo yetu,” amesema Ally Kamwe.

Kamwe amesema kuwa uzinduzi wa Tamasha hilo ambalo kilele chake ni Septemba 12, 2025 utafanyika kesho Dar es Salaam.

“Uzinduzi huu utafanyika katika Viwanja vya Zakhem Mbagala kuanzia saa 5:00 asubuhi. Na hapa nizungumze na Wanachama na Mashabiki wa Yanga, kesho tunataka Dar es Salaam ibadilike, iwe kijani na njano.

“Uzinduzi wa Wiki ya Mwananchi haujafanyika Dar es Salaam kwa muda mrefu. Kesho mtaona pande zote za Dar es Salaam zikielekea pale Zakhem wakipambwa na kijani na njano. Kwenye shughuli hiyo ya kesho, tutatambulisha baadhi ya wasanii ambao watatumbuiza katika kilele cha Wiki ya Mwananchi,” amesema Kamwe.

Kamwe ametamba kuwa msimu huu wamefanya usajili wa wachezaji wenye ubora wa hali ya juu ambao utaifanya iendelee kuwa tishio na kutetea mataji yake.

“Uzuri wa timu yetu, wachezaji ambao wapo timu ya taifa, hata kama Hemed Morocco ataamua akae nao kwenye timu ya taifa mwaka mzima, Yanga itakuwa tishio tu.