Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe ameshiriki mkutano na wadau wa korosho uliokuwa ukijadili maandalizi ya msimu wa zao hilo la biashara kwa mwaka 2024 / 2025 uliofanyika mkoani Mtwara, Septemba 30, 2025. Kabla ya kuhudhuria mkutano huo Bashe alikwenda katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Patrick Sawala na kupata taarifa ya hali ya kilimo ya mkoa huo. Picha na Edwin Mjwahuzi