Mwili wa Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania, Edward Lowassa umezikwa nyumbani kwake, Kijiji cha Ngarash, Wilaya ya Monduli, Mkoa wa Arusha mchana wa leo huku nyuso za simanzi zikitawala kwa waombolezaji wakati jeneza lenye mwili wa mpendwa wao ukishushwa kaburini. Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na viongozi waandamizi wa serikari na vyama vya siasa waliungana na familia na wananchi kutoa maeneo mbalimbali katika ibada ya mazishi ya kiongozi huyo. Picha na Said Khamis na Ikulu