Mbunge wa Kilombero (CCM), Abubakar Asenga amemuomba Serikali ikamsaidie kupima ardhi ya wananchi ili akwepe laana ya Askofu.
Asenga ametoa kauli hiyo Alhamisi Mei 25,2023 wakati akichangia Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Asenga amesema katika jimbo lake kuna mgogoro wa siku nyingi kati ya wananchi na Kanisa Katoliki ambao unahitaji busara ya Serikali baada ya Askofu kuamua kuacha mgogoro.