Rais Samia Suluhu Hassan leo Agosti 15, 2024 amewaapisha viongozi mbalimbali wakiwemo mawaziri wanne, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga, Wakili Mkuu wa Serikali manaibu katibu wakuu wa wizara, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) pamoja na jaji wa Mahakama ya Rufaa. Hafla hiyo ya kuapisha viongozi hao imefanyika Ikulu ya Dar es Salaam.