Klabu ya Yanga imeanza vyema katika mashindano ya Kimataifa katika mechi ya hatua ya awali Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) ikiibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Asas FC ya Djibouti katika Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam.
Mabao ya mchezo huo yalifungwa na Steohane Aziz KI dakika ya 22 na Kenedy Musonda dakika ya 53.
Mchezo wa marudiano baina ya timu hizo utachezwa Agosti 26 kwa ajili ya kupata mshindi atakayecheza hatua ya kwanza CAFCL.