Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

 Mwana FA aipongeza Benki ya CRDB kwa kuendeleza vipaji vya vijana nchini

Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Michezo, Habari, Sanaa na Utamaduni, Hamis Mwinjuma ‘ Mwana FA’ ameipongeza Benki ya CRDB kwa jitihada zake za kuendelea kuwekeza katika maendeleo ya vijana kupitia michezo, elimu ya fedha na uwezeshaji wa kiuchumi kama sehemu ya mchango wake katika kukuza uchumi jumuishi na maendeleo ya Taifa.

Mwinjuma ametoa pongezi hizo kwenye kilele cha mashindano ya CRDB Bank Nanauka Cup zilizofanyika zilizofanyika katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.

Katika fainali hiyo, timu ya Naliendele FC iliibuka kidedea katika fainali hizo baada ya kuibwaga Vigaeni FC kwa mabao 3-0 na kuzawadiwa kombe na kitita cha Sh milioni 3. 

Alisema kuwa benki ya CRDB ni taasisi kubwa ya fedha yenye maono ya kuendeleza vijana kupitia sekta ya michezo na Sanaa ambapo hivi karibuni ilidhamini mashindano ya kusaka vipaji kwa wanamuziki ya Bongo Star Search.

“Ni furaha kwa kila mdau kuona kwamba inawashika vijana kupitia michezo na burudani. Leo tupo hapa Mtwara tukishuhudia fainali ya (CRDB Bank) Nanauka Cup lakini nafahamu kwamba mnadhamini mashindano mengine yanayowahusisha vijana. Hongereni sana Benki ya CRDB,” alisema Mwinjuma.

Kutokana na vipaji vilivyoonyeshwa na wachezaji kwenye mashindano hayo yaliyoanza Juni 13, Mwinjuma amesema Mkoa wa Mtwara una vipaji vingi na vikubwa vya mpira wa miguu hivyo ni wakati sasa kwa wadau kushirikiana kuhakikisha mkoa huo unapata uwakilishi kwenye Ligi Kuu ili kuendeleza ari ya vijana nchini.

Akizungumza katika  fainali hizo, Kaimu Mkurugenzi wa Wateja Wadogo na wa Kati wa Benki ya CRDB, Mshindo Magimba alizipongeza timu zote 18 za jimbo la Mtwara mjini zilizoshiriki katika mashindano.

Magimba alisema kuwa yamekuwa jukwaa muhimu la kuibua na kukuza vipaji vya michezo, kuimarisha mshikamano  wa jamii na kuwafikia vijana kwa elimu ya fedha pamoja na fursa za kiuchumi.

“Benki ya CRDB tunaamini vijana ni nguvukazi muhimu ya maendeleo ya Taifa ndiyo maana tunaendelea kuwafuata mahali walipo na kuwekeza katika sekta mbalimbali ikiwemo michezo, sanaa, ubunifu, ujasiriamali na uzalishaji ili kuwaunganisha na fursa za kujikwamua kiuchumi,” amesema.

Katika uwezeshaji wananchi kiuchumi, mpaka sasa Benki ya CRDB imetoa mikopo yenye thamani ya zaidi ya shilingi trilioni 15 kwa wajasiriamali wa sekta mbalimbali nchini, hivyo kuchangia kukuza biashara, kuongeza kipato cha wananchi na kuimarisha uchumi wa Taifa.

Magimba amesema ushiriki wa Benki ya CRDB katika michezo na burudani unadhihirishwa na udhamini wake katika mashindano na matukio mbalimbali ikiwemo CRDB Bank Federation Cup, iMbeju-Ndondo Cup, CRDB Bank Taifa Cup, Zuchu-Imbeju Masterclass na CRDB Bank Bongo Star Search, ambayo yote yanalenga kutoa fursa kwa vijana.

Mashindano hayo yanaandaliwa na Mbunge wa Mtwara Mjini ambaye ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais anayeshughulikia Maendeleo ya Vijana, Mheshimiwa Joel Nanauka ili kuongeza ushirikiano kwa wananchi wa Mtwara sambamba na kupata fursa ya kujadili maendeleo ya jimbo hilo.

Nanauka naye ameishukuru Benki ya CRDB kwa kudhamini mashindano hayo ambapo kwa sasa yamekuwa maarufu nchini.