Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Baduel atimkia Chaumma, atiania kuwania ubunge Bahi

Katika picha, Omari Baduel, aliyekuwa Mbunge Bahi 2010-2020, akionesha kadi ya Chaumma baada ya kukabidhiwa leo alipojiunga rasmi Chaumma mjini Bahi.

Muktasari:

  • Baduel aliyekuwa mbunge Bahi kwa miaka 10 ajiunga Chaumma huku akiomba ridhaa ya kuwania ubunge kwenye jimbo hilo.


Dodoma. Mbunge wa zamani wa Bahi (CCM), Omari Baduel, amekihama chama hicho na kujiunga Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma).

Baduel ambaye amekuwa mbunge kwa miaka 10 mfululizo kupitia CCM, amejiunga na Chaumma leo Alhamisi Agosti 21, 2025 katika mkutano wa hadhara wa mtiania wa urais wa Tanzania wa chama hicho, Salum Mwalimu.

Mbunge huyo aliyeingia bungeni mwaka 2010 na kudumu kwa vipindi viwili hadi 2020, amepokewa na uongozi wa Taifa wa Chaumma katika mkutano huo uliofanyika mjini Bahi kwa lengo la kutafuta wadhamini.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa kadi ya chama hicho,  Baduel amesema ameamua kutafuta jukwaa jipya la siasa.

Katika picha, Omari Baduel, aliyekuwa Mbunge Bahi 2010-2020, akionesha kadi ya Chaumma baada ya kukabidhiwa leo alipojiunga rasmi Chaumma mjini Bahi.

"Nimekuwa mbunge wenu hapa, mnanifahamu vizuri, leo najiunga rasmi na Chaumma kuendeleza mapambano ya kuwatetea," amesema.

Akieleza hatima yake ya kisiasa kufuatia uamuzi huo, Baduel ameweka nia na amechukua fomu ya kugombea ubunge wa jimbo hilo kupitia chama chake hicho kipya.

Akizungumza baada ya kumpokea mwanachama huyo mpya, Makamu Mwenyekiti wa Chaumma Bara, ambaye pia ni mgombea mwenza wa urais wa chama hicho, Devotha Minja amemmwagia sifa mwanasiasa huyo akisema anamfahamu vyema.

"Ndugu zangu wanabahi mmepata jembe, Baduel ninamfahamu, nimekuwa naye bungeni, huyu ni mtu makini hakika atawatetea wanabahi," amesema na kuongeza;

"Kwa miaka 64 yote tangu uhuru, vijana wameendelea kukosa ajira, miaka 64 vijana wameendelea kutegemea pikipiki za mkopo ili watafute  pesa, tupeni mbunge wa Chaumma, tupeni diwani wa Chaumma,  tupeni rais wa Chaumma tunakwenda kumaliza tatizo hili,"  amesema.