Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chalamila avutiwa na ubunifu wa Yas katika Maonesho ya Sabasaba

Dar es Salaam. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila ameipongeza kampuni ya mawasiliano ya Yas kwa kupanua upatikanaji wa huduma za kidijitali na kifedha kupitia suluhisho bunifu zilizooneshwa katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (DITF), maarufu kama Sabasaba.

Chalamila alitoa kauli hiyo baada ya kutembelea banda la Yas katika viwanja vya Sabasaba, Barabara ya Kilwa, ambako alipatiwa maelezo na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Pierre Bacara, kuhusu bidhaa na huduma mbalimbali zinazolenga kuboresha maisha ya Watanzania.

Katika ziara hiyo, Chalamila aliipongeza Yas kwa kutengeneza suluhisho zinazolenga kukidhi mahitaji ya jamii, akisema ubunifu wa kampuni hiyo unasaidia kuboresha upatikanaji wa huduma za mawasiliano ya kidijitali, afya na ujumuishaji wa kifedha.

“Suluhisho mbalimbali zinazooneshwa hapa, ikiwemo huduma ya uchunguzi wa macho bure, mpango wa kumiliki simu janja kwa gharama nafuu, intaneti yenye kasi kubwa na huduma za kifedha kidijitali, zinaonesha namna ubunifu unavyoweza kubadilisha maisha ya watu huku ukiwawezesha wajasiriamali, familia, wanafunzi na wafanyabiashara,” alisema.

Alitaka Yas kuendelea kuwekeza katika ubunifu unaolenga jamii, akisema suluhisho zinazotumia teknolojia zina umuhimu mkubwa katika kutatua changamoto za kila siku, kuboresha maisha ya wananchi na kuanzisha fursa mpya za kiuchumi.

Kwa upande wake, Bacara alisema kampuni hiyo inaendelea kuwekeza katika teknolojia na huduma zinazozingatia mahitaji ya wateja kwa lengo la kukuza ujumuishaji wa kidijitali, uwezeshaji wa kifedha na kuboresha mawasiliano kwa watu binafsi, wafanyabiashara na taasisi.

Moja ya huduma zilizovutia wananchi katika banda la Yas ni uchunguzi wa macho bure, ambao umevutia idadi kubwa ya wageni wanaopata fursa ya kufanyiwa vipimo na wataalamu wa afya ya macho.

Alisema mpango huo ni sehemu ya jitihada za kampuni kusaidia huduma za afya kwa jamii na kutoa huduma zenye thamani kwa wananchi wakati wa maonesho hayo ya kila mwaka.

Bacara alisema Yas pia inatoa mpango wa kuwawezesha wateja kumiliki simu janja na rauta za 5G kupitia mfumo wa malipo rahisi kwa awamu, jambo linalowawezesha Watanzania wengi zaidi kupata huduma za intaneti yenye kasi bila kulipa gharama yote kwa wakati mmoja.

Katika banda hilo, wageni pia wanapata fursa ya kufahamu huduma ya Yas Fiber, inayotoa intaneti yenye kasi kwa matumizi ya nyumbani, wajasiriamali na biashara, huku ikiwezesha kazi kwa njia ya mtandao, masomo mtandaoni na ukuaji wa biashara.

Kwa wateja wa kampuni na taasisi, Yas Business inaonesha suluhisho mbalimbali za kidijitali zinazolenga kuboresha mawasiliano, ufanisi na uzalishaji katika shughuli za biashara.

Aidha, jukwaa la huduma za kifedha la kampuni hiyo, Mixx, linaonesha huduma za kifedha kidijitali ikiwemo miamala ya fedha kwa njia ya simu, malipo na huduma za kuweka akiba zinazolenga kurahisisha upatikanaji wa huduma za kifedha.

Bacara alisema Yas itaendelea kutengeneza bidhaa na huduma bunifu zinazokidhi mabadiliko ya mahitaji ya Watanzania huku ikiunga mkono ajenda ya taifa ya mageuzi ya kidijitali.

Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam yamewakutanisha mamia ya waoneshaji wa ndani na nje ya nchi, yakitoa fursa kwa kampuni mbalimbali kuonesha bidhaa zao, kukutana na wateja na kujenga ushirikiano wa kibiashara.

Yas imesema ushiriki wake katika Sabasaba unaonesha dhamira yake ya kuendelea kutoa suluhisho zinazotumia teknolojia kuboresha maisha ya wananchi na kuchangia maendeleo ya kiuchumi ya Tanzania.