Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Cheyo aongoza mkutano mkuu wa UDP mgombea urais, mwenza kujulikana leo

Mwenyekiti UDP Taifa,John Cheyo akiwasili kwenye ukumbi kwaajili ya uchaguzi Mkuu wa chama hicho,jijini Dar es Salaam leo. Picha na Michael Matemanga

Muktasari:

  • Cheyo, maarufu Mzee Mapesa, amewasili ukumbini hapo saa sita mchana akiwa amevalia suti ya buluu na anatembelea mkongojo, huku akisaidiwa na watu wawili.

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chama cha United Democratic Party (UDP), John Cheyo leo Jumatatu Agosti 11, 2015, amehudhuri­a mkutano mkuu wa chama hicho unaofanyika katika Ukumbi wa Lulu, Sinza, jijini Dar es Salaam, licha ya changamoto za kiafya zinazomkabili kwa muda mrefu.

Cheyo, maarufu Mzee Mapesa, amewasili ukumbini hapo saa sita mchana akiwa amevalia suti ya buluu, anatembelea mkongojo, huku akisaidiwa na watu wawili.

Akihutubia wajumbe, Cheyo amesema kama si umuhimu wa mkutano huo asingetoka kitandani.

“Kama isingekuwa kikao hiki, nisingeondoka kitandani. Lakini kwa sababu UDP ni chama cha upendo,  pamoja daima imebidi hata kwa mkongojo nije,” amesema Cheo.

Amesema amefurahishwa na wingi wa wajumbe licha ya changamoto za kifedha zinazokikabili chama hicho, akibainisha kuwa baadhi ya wanachama wamejitolea kugharamia nauli zao ili kushiriki mkutano mkuu huo muhimu.

“Nawashukuru sana viongozi na wanachama wetu. Kwa shida mbalimbali mmejitolea hata nauli zenu kuja kwenye kikao. Chama ni watu na kama hakina watu hakiwezi kuwa chama. Ninamwambia Msajili wa Vyama vya Siasa ajue chama kipo na watu ni hawa,” amesema Cheyo.

Kuhusu malengo ya mkutano huo, Cheyo amesema agenda kuu ni kutimiza takwa la kisheria la kumuidhinisha mgombea urais wa chama na mgombea mwenza, ambapo kamati kuu itathibitisha jina, kabla ya kuwasilishwa kwa mkutano mkuu maalumu kwa ajili ya kuridhiwa.

Aidha, amewashukuru wawakilishi wa vyama vingine vya siasa walioitikia mwaliko, akisema  kuwa hali hiyo ni ishara ya mshikamano.

“Msituchoke tukiimba wimbo huu wa ‘upendo, daima, pamoja,’ kwa sababu nchi hii ni yetu. Hatuna mahali pengine pa kukimbilia. Tanzania tuendelee kuiweka salama na yenye amani,” amesema kiongozi huyo.

Mbali na wajumbe wa UDP, mkutano huo unahudhuriwa pia na wawakilishi kutoka vyama vya UPDP, Ada-Tadea, Demokrasia Makini, SAU na NCCR-Mageuzi.

Baada ya ufunguzi wa mkutano, wajumbe wametolewa nje ili kuruhusu kikao cha kamati kuu kuendelea.

Baadaye, mkutano mkuu utaendelea kwa ajili ya kutajiwa rasmi jina la mgombea urais na mgombea mwenza wa chama hicho.

Endelea kufuatilia mitandao yetu kwa habari zaidi.