Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dk Tulia awapa matumaini ya ushindi CCM, aahidi ujenzi wa soko la kisasa Nsalaga

Muktasari:

  • Kauli hiyo ameitoa leo Jumatatu Septemba 22,2025 wakati wa mkutano  wa kampeni  uliofanyika  katika viwanja  vya Shule ya Msingi  Itezi Kata ya Nsalaga Jijini Mbeya.

Mbeya. Mgombea ubunge Uyole Mkoa wa Mbeya, Dk Tulia Ackson amesema wakati wa hesabu kura za  Chama cha Mapinduzi  (CCM), umefika na  kutaja  kipaumbele ni ujenzi wa soko la kisasa la Nsalaga ili kuchochea  shughuli  za  kiuchumi  kwa wajasiriamali.

Mbali na uwekezaji wa Soko, pia amesema Serikali imeweza kutekeleza ilani ya uchaguzi 2020/25 kwa kuondoa hadha ya watoto kukaa chini katika shule za msingi na Sekondari kwenye Mbeya Mjini na Uyole kabla halijatangazwa kuwa Jimbo jipya.

Hatua hiyo imetajwa ni kupunguza  mzigo kwa wananchi na  wazazi kuchangia  elimu na shughuli za kiuchumi.

Dk Tulia amesema jana Jumatatu  Septemba 22, 2025 katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Itezi Kata ya Nsalaga.

"Umefika wakati wa CCM kuhesabu kura na kusema yaliyo fanywa na Rais Samia Suluhu Hassan katika sekta  mbalimbali  za elimu, afya na maji na barabara katika kupiga hatua za maendeleo," amesema.

Amesema awali kabla ya Serikali kugawanya Jimbo  jipya la Uyole aliweza kutumikia kata 36 hizi 13 zilizobaki atazicharaza kwa  kuleta  maendeleo.

Katika hatua nyingine,  Dk Tulia amesema binafsi amemshukuru Rais Samia kwa kuridhia kuanzisha Jimbo jipya la Uyole na kuwaondoa hofu wananchi maendeleo  yataletwa kwa kasi.

Amesema ilani ya uchaguzi 2020/ 2025 mpaka 2030  imeelekeza kila kata zenye idadi kubwa ya watu kujengwa vituo vya afya lengo ni kusogeza  huduma bora  kwa jamii.

"Jamani mambo makubwa yanakuja kazi yenu  ni kumpa kura za kishindo  mgombea  Urais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Samia Suluhu  Hassan  Oktoba 29,2025, amesema ," amesema.

Sambamba na hilo amesema ataendelea  kuboresha utoaji wa bima za afya kwa wananchi  wenye uhitaji .