Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Halotel, Vietnam wakabidhi kompyuta Sekondari Kiwanja cha Ndege

Mkuu wa Huduma za Fibre wa Halotel Dodoma, Steve Komu (wa kwanza kulia), akitoa maelezo kwa mmoja wa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kiwanja cha Ndege iliyopo Dodoma, baada ya kampuni hiyo kutoa msaada wa kompyuta kwa shule hiyo.

Muktasari:

  • Kampuni ya Mawasiliano ya Halotel kwa kushirikiana na Ubalozi wa Vietnam nchini Tanzania imekabidhi vifaa vya kompyuta na kukarabati maabara ya TEHAMA katika Shule ya Sekondari Kiwanja cha Ndege, Dodoma, hatua inayolenga kuwawezesha wanafunzi kupata elimu ya kidijitali na kuongeza ujuzi wa teknolojia.

Dodoma. Kampuni ya Mawasiliano ya Halotel kwa kushirikiana na Ubalozi wa Jamhuri ya Kisoshalisti ya Vietnam nchini Tanzania, wamekabidhi vifaa vya kompyuta na kukarabati maabara ya Tehama katika Shule ya Sekondari Kiwanja cha Ndege iliyopo Jijini Dodoma.

Vifaa hivyo vilikabidhiwa Jumamosi, Juni 20, 2026, ikiwa ni sehemu ya mpango wa Uwajibikaji kwa Jamii wa Kampuni (CSR), unaolenga kuboresha mazingira ya kujifunzia na kuwawezesha wanafunzi kupata maarifa ya kidijitali.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Halotel, Tran Thuy Dung, alisema maabara hiyo iliyoboreshwa itawanufaisha mamia ya wanafunzi kwa kuwapatia mazingira bora ya kujifunza Tehama pamoja na upatikanaji wa rasilimali za kujifunzia mtandaoni.

Balozi wa Vietnam hapa nchini, Vũ Thanh Huyền akizingumza wakati wa hafla ya kukabidhi kompyuta pamoja na vifaa vyake kwa Sekondari ya Kiwanja cha Ndege iliyopo Dodoma.

Alisema maabara hiyo imewekewa kompyuta mpya pamoja na huduma ya intaneti ya uhakika, jambo litakalosaidia wanafunzi kujenga ujuzi unaohitajika katika uchumi wa kisasa unaotegemea teknolojia.

“Sisi kama Halotel tunaamini kuwapata teknolojia ni kupata fursa. Maabara hii ya kompyuta si zawadi ya vifaa pekee, bali ni uwekezaji katika mustakabali wa wanafunzi hawa na mageuzi ya kidijitali ya Tanzania,” alisema Dung.

Aliongeza kuwa ushirikiano huo na Ubalozi wa Vietnam unaonyesha dhamira ya pamoja katika kusaidia elimu na maendeleo ya jamii.

Kwa upande wake, Mkuu wa Shule ya Sekondari Kiwanja cha Ndege, Daniel Mpagame, aliishukuru Halotel na Ubalozi wa Vietnam kwa msaada huo akisema utasaidia wanafunzi kuongeza uelewa na kupata maarifa zaidi kupitia teknolojia.

Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mawasiliano ya Halotel, Tran Thuy Dung (kushoto), akikabidhi kompyuta na vifaa vyake kwa Mkuu wa Shule ya Sekondari Kiwanja cha Ndege, Daniel Mpagame (kulia).

“Maabara hii iliyokarabatiwa na upatikanaji wa intaneti itasaidia wanafunzi wetu kujifunza na kupata maarifa zaidi,” alisema Mpagame.

Alisema msaada huo una umuhimu mkubwa kwa mustakabali wa wanafunzi na jamii ya shule kwa ujumla.

Mradi huo ni sehemu ya jitihada endelevu za Halotel katika kuchangia ujumuishi wa kidijitali nchini Tanzania, ambapo kampuni hiyo imeeleza kuendelea na mipango kama hiyo katika shule mbalimbali nchini.

Hafla ya makabidhiano ilihudhuriwa na wawakilishi wa Halotel, maofisa wa Ubalozi wa Vietnam, wawakilishi wa Wizara ya Mambo ya Nje, viongozi wa Serikali, viongozi wa CCM, uongozi wa shule, wanafunzi na wanajamii.