Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kampeni ya Mixx kombe la dunia yashika kasi

Mkurugenzi wa Biashara wa Mixx, James Sumari (katikati), akisherehekea pamoja na washindi wa kampeni ya Kila Muamala ni Bao la Ushindi, Sabdiki Vike (kulia) na Benson Mbile (kushoto), baada ya kila mmoja kujishindia Shilingi milioni 1 katika droo ya pili ya kampeni hiyo. Kampeni inalenga kuhamasisha matumizi ya huduma za kifedha kidijitali huku ikiwazawadia wateja wanaotumia huduma za Mixx.

Kampuni ya Mixx imejivunia kuendelea kuongezeka kwa idadi ya wateja wake pamoja na matumizi ya huduma zake za kifedha kidijitali kufuatia mwitikio mkubwa wa Watanzania katika kampeni ya “Kila Muamala ni Bao la Ushindi”, inayofanyika kwa ushirikiano na kampuni ya Hisense ikiwa na lengo la kutoa zawadi na kuwapeleka Watanzania kwenda kutazama michuano ya Kombe la Dunia inayofanyika nchi za Marekani, Mexico na Canada.

Akizungumza wakati wa droo ya pili ya kampeni hiyo, Mkurugenzi wa Biashara wa Mixx, James Sumari, amesema kampeni hiyo imekuwa kichocheo muhimu katika kuhamasisha matumizi ya njia rasmi za malipo ya kidijitali, huku idadi ya watumiaji wa huduma hiyo ikiendelea kuongezeka nchini.

Sumari amesema moja ya mafanikio makubwa yaliyopatikana katika kipindi hicho ni kuongezeka kwa matumizi ya Mixx Super App, ambayo Watanzania zaidi ya milioni moja wanatumia App hiyo lakini ikichangiwa kwa kiasi kikubwa na mwitikio wa mashabiki kuhusu fainali za Kombe la Dunia mwaka huu.

Ameeleza kuwa matumizi ya huduma za kidijitali kama Mixx yanasaidia kuimarisha usalama wa fedha za watumiaji, kupunguza utegemezi wa fedha taslimu na kuwezesha ufuatiliaji wa matumizi ya kifedha kwa urahisi zaidi kwa watu binafsi na wafanyabiashara.

Wakizungumza baada ya kupokea zawadi zao, baadhi ya washindi wa kampeni hiyo wamesema ushindi huo umewapa hamasa zaidi ya kuendelea kutumia huduma za Mixx katika shughuli zao za kila siku lakini pia wakiwa na matumaini makubwa kuwa wanaweza kuwa baadhi ya washindi watakaokwenda kutazama michuano hiyo mikubwa zaidi duniani.

Mmoja wa washindi hao, Sabdiki Vike, amesema alipokea taarifa za ushindi wake kwa mshangao mkubwa kwani awali alidhani ni utani au jaribio la utapeli. Hata hivyo, baada ya kuwasiliana na kampuni na kufika katika makao makuu yao alithibitisha kuwa alikuwa mshindi halali wa kampeni hiyo.

Kwa upande wake, Benson Benjamin amesema Mixx imekuwa msaada mkubwa katika kufanya miamala yake kwa usalama na urahisi zaidi.

Jumla ya washindi 20 walipatikana katika droo hiyo, wakitoka katika mikoa mbalimbali ikiwemo Dar es Salaam, Zanzibar, Arusha na maeneo mengine ya nchi. Mbali na washindi wa fedha taslimu wa shilingi milioni moja moja kila siku, baadhi yao pia walijishindia vifaa mbalimbali vya nyumbani kutoka Hisense, ikiwemo televisheni ya inchi 55, spika na jokofu, baada ya kutumia huduma za Mixx kufanya miamala.

Lengo la pili la Kampeni ya “Kila Muamala ni Bao la Ushindi” inalenga kuhamasisha matumizi ya huduma za kifedha kidijitali huku ikiwazawadia wateja wanaofanya miamala kupitia Mixx, safari ya kwenda Mexico kushuhudia mechi za Kombe la Dunia la FIFA mubashara kwa washindi 5, na zawadi kuu ya Kampeni ya shilingi milioni 50.