Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kifo cha Ndugai charudisha mchakato kura za maoni Jimbo la Kongwa

Muktasari:

  • Katibu wa CCM Wilaya ya Kongwa, Joyce Mkaugala amesema mchakato wa kuchukua fomu utafanyika kwa siku moja.

Dodoma. Kufuatia kifo cha aliyeongoza kura za maoni Jimbo la Kongwa kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Job Ndugai, kura hizo sasa zitapigwa upya Jumapili Agosti 17, 2025.

Katika matokeo ya awali, Ndugai aliongoza kwa kupata kura 5,692, akifuatiwa na  Isaya Mngurumi (2,602), Deus Seif (1,260), Dk Samora Mshang’a (544), Dk Simon Ngatunga (517), Elias Mdao (435), Philip Chiwanga (558), Paschal Mahinyila (331), Balozi Emmanuel Mbennah (232) na Ngaya Mazanda aliyepata kura 195.

Katibu wa CCM Wilaya ya Kongwa, Joyce Mkaugala amesema mchakato wa kuchukua fomu utafanyika kwa siku moja ambayo ni leo Jumanne Agosti 12, 2025.

Mkaugala amesema na kura zitapigwa leo kwa utaratibu wa wajumbe ngazi ya kata kama ilivyofanyika Agosti 4, 2025 na baadaye vikao vya kawaida vitaendelea.

"Ni kweli tunatoa fomu kwa siku moja ya leo (Agosti 12,2025) baada ya hapa tunaendelea na taratibu za kawaida ambapo Jumapili ya terehe 17,2025 wajumbe watapiga kura za maoni," amesema Mkaugala.

Katibu amesema gharama za fomu ni kama ilivyokuwa awali, watalipia Sh500,000 na si vinginevyo.

Hata hivyo, hakuweka wazi kama kutakuwa na kampeni za kuzunguka kwa wajumbe kwa ajili ya kuwanadi wagombea kama awali akisema wanachama wasubiri wataelezwa utaratibu.

Wilaya ya Kongwa ilizaliwa kutoka Wilaya ya Mpwapwa katika mkoa wa Dodoma na kwa sasa inaundwa na Wilaya 22.

Sifa pekee inayoitambulisha Wilaya hii ni soko Kuu la mazao ya mshindi la Kibaigwa, makumbusho ya wapigania Uhuru ikiwemo handaki kubwa la Samora Machel na wingi wa matrekta unaotajwa unazidi maeneo mengi nchini.