Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mawakili wa serikali kuzindua kitabu cha 'Falsafa ya Sheria ya Mama Samia'

Dar es Salaam. Chama cha Mawakili wa Serikali Tanzania kinatarajia  kuzindua kitabu, walichokipa jina la 'Falsafa ya Sheria ya Mama Samia' huku mgeni rasmi akitarajiea kuwa Waziri Mkuu, DK Mwigulu Nchemba.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi Julai 9 2026 ,Makamu wa Rais wa chama hicho, Deborah Mchalo, amesema  kitabu hicho kimeandaliwa kwa lengo la kuelezea kwa kina, kwa ushahidi na takwimu, namna sheria mbalimbali zilizotungwa nchini zilivyochangia kuleta mafanikio makubwa katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii.


Kwa mujibu wa Debora   kutokana na wingi wa sheria zilizopo nchini, waandishi waliamua kujikita katika uchambuzi wa sheria zilizotungwa kuanzia mwaka 2021, kipindi cha Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais  Samia Suluhu Hassan na ndio maana wakakipa jina la Falsafa ya Sheria ya Mama Samia.

"Kitabu hicho kinachambua mageuzi makubwa ya kisheria yaliyofanyika tangu mwaka 2021 hadi sasa, yakihusisha sekta mbalimbali ikiwemo uwekezaji, kodi, elimu ya juu, ardhi, nishati na maeneo mengine muhimu ya maendeleo,"amefafanua.

Makamu huyo ameleza kuwa k uchambuzi uliomo katika kitabu umefanywa na mawakili waliobobea katika taaluma ya sheria, kwa lengo la kuweka kumbukumbu ya mchango wa mageuzi ya kisheria katika kuimarisha utawala bora na kuchochea maendeleo ya Taifa.

Katika hatua nyinginr,chama hicho kimeeleza kutarajia 
 kifanya Mkutano wake mkuu wa mwaka, utakaowakutanisha wanachama kujadili masuala mbalimbali yanayohusu maendeleo ya taaluma ya sheria, utendaji wa chama na mchango wa mawakili wa serikali katika kuimarisha utoaji wa haki nchini.

Katibu wa chama hicho, Rashid Said, amesema kitabu hicho kinaeleza namna maboresho ya kisheria yalivyowezesha maendeleo katika sekta mbalimbali ikiwemo uwekezaji, nishati, mawasiliano, habari na maeneo mengine muhimu ya uchumi.


Said amesema maendeleo ya nchi yoyote hayawezi kupatikana bila kuwa na mfumo madhubuti wa sheria zinazotungwa na kutekelezwa kwa ufanisi, ndiyo maana mawakili wa serikali kupitia chama chao waliamua kukusanya na kuandika mafanikio yaliyopatikana chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Kwa mujibu wa Rashid, kitabu hicho hakijajikita katika uchambuzi wa sheria pekee, bali pia kinaangazia sera na maamuzi ya kimkakati yaliyowezesha Tanzania kupata mafanikio katika nyanja za uchumi na ustawi wa jamii.

Kwa upande wake, Mweka Hazina wa chama hicho, Andrew Kevela, amesema zaidi ya mawaziri 10 wanatarajiwa kushiriki katika uzinduzi wa kitabu hicho, jambo litakalotoa fursa kwa wananchi, mawakili na wadau wengine kukutana na viongozi mbalimbali wa serikali pamoja na kujadili masuala yanayohusu maendeleo ya sekta ya sheria na utawala bora.