Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mgombea udiwani Mwasanga aahidi kuanza na barabara

Mgombea udiwani Kata ya Mwasanga kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Brandy Nelson (kulia) akiwapungia mkono  wananchi wakati akiomba ridhaa (kushoto), Mjumbe wa Kamati Kuu  ya Halmashauri  Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk Tulia Ackson. Picha na Hawa Mathias.

Muktasari:

  • Brandy Nelson amesema bado kuna changamoto ya barabara ya kufika katika Soko la Isoso jambo ambalo ni changamoto kwa wajasiriamali wa mbogamboga kuyafikia masoko ya mjini.

Mbeya. Mgombea udiwani Kata ya Mwasanga kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Brandy Nelson amewaomba wananchi kumpa ridhaa ili aweze kutatua changamoto mbalimbali ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya barabara, ili kurahisisha wajasiriamali wa mboga mboga kuyafikia masoko ya mjini.

Brandy ametoa kauli hiyo leo Septemba 13, 2025 wakati wa akizindua mkutano wa kampeni na kunadi sera katika viwanja vya Shule ya Msingi Mwasanga.

Uzinduzi huo umefanywa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya  CCM na mgombea ubunge Uyole, Dk Tulia Ackson.

Brandy amesema endapo atapata ridhaa atahakikisha Kata hiyo inapiga hatua za maendeleo.

"Hii ni mara yangu ya kwanza kuomba ridhaa kutumikia nafasi ya udiwani nawaombeni mniamini niweze kuwatumikia, lakini pia nimeona changamoto ya barabara ambayo ni kero kwa wajasiriamali wa mbogamboga na wananchi," amesema.

Amesema mbali na kuomba ridhaa ya kuwatumikia wananchi, pia Dk Tulia Ackson ameleta maendeleo hususan ujenzi wa daraja kubwa la Mwasanga ambalo liligharimu maisha ya Watanzania kutokana na mafuriko.

"Wananchi hawana mashaka na Serikali ya CCM, lakini niwaeleze wazi nitaendeleza kunadi sera ya ilani ya uchaguzi 2025/30 kuhakikisha mkakati wa Rais Samia Suluhu Hassan ya Kazi na Utu inatekelezwa kwa vitendo," amesema.

Amesema kwa sasa Serikali imefungua sekta ya usafirishaji kwa kuwepo na usafiri wa bajaji na bodaboda, lakini kutokana na changamoto ya ubovu wa barabara wanashindwa kuwafikia wajasirimali na wananchi wa maeneo ya pembezoni.

Kwa upande wake Dk Tulia, ameomba wananchi kuchagua viongozi wa CCM, kuanzia nafasi ya Rais, ubunge na udiwani huku kwa Kata ya Mwasanga wampe mtiania husika.

Amesema Serikali imefanya mambo makubwa katika Kata ya Mwasanga hakuna changamoto ya uhaba wa vyumba vya madarasa na madawati kwa shule za msingi na sekondari ikiwemo wanafunzi kukaa chini.

"Sio tu tumemaliza tatizo la madawati, lakini pia hakuna mzazi ambaye atachangia madawati, sambamba na mfumo wa watoto wanaochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza kusoma kwa awamu kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa Serikali imemaliza vyote," amesema.