Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mkwakwani yang’ara viti 1800 vyafungwa, CCM yasistiza kukamilisha ukarabati

New Content Item (4)

Muktasari:

  • Ukarabati wa Uwanja wa CCM Mkwakwani wafikia asilimia 40, viti 6,500 vilivyokuwa vimetelekezwa sasa vimefungwa huku mpango ukiwa kuongeza vingine 2,500.

Tanga. Zoezi la kufunga viti na ukarabati katika Uwanja wa CCM Mkwakwani limefikia asilimia 40, huku jumla ya viti 1, 800 vilivyokuwa vimetelekezwa kwa muda mrefu sasa vikiwa tayari vimefungwa, hatua inayozidi kuimarisha mazingira rafiki na yanayokubalika kwa michezo ya soka.

Kwa muda mrefu, uwanja huo ulikuwa katika hali isiyoridhisha kutokana na uwepo wa viti hivyo 6, 500 ambavyo havikuwa vimefungwa pamoja na changamoto nyingine za miundombinu, hali iliyosababisha kushindwa kukidhi vigezo vya michezo ya ushindani na kuathiri timu za mkoa wa Tanga.

Kutokana na hali hiyo, uongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tanga ulichukua hatua za haraka, ikiwa ni pamoja na kuwajibishwa kwa aliyekuwa meneja wa uwanja huo, Akida Machai, kwa kushindwa kusimamia ipasavyo utekelezaji wa maboresho hayo.

Baada ya hatua hizo, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga, Rajab Abdalah, amefanya ziara yake ya pili ya ukaguzi katika uwanja huo Aprili 10, 2026 ili kujionea maendeleo ya kazi.

New Content Item (4)

Akizungumza mara baada ya ukaguzi huo, amesema ameridhishwa na kasi ya ufungaji wa viti na kusisitiza kuwa kazi itaendelea hadi kukamilika kwa mpango wa kuongeza viti vingine 2,500 ili kukidhi mahitaji yote ya uwanja.

“Hatukubaliani kabisa na uzembe wa kuacha viti bila kufungwa wakati uwanja unahitaji maboresho. Lazima tukamilishe kazi hii kwa wakati ili kurejesha hadhi ya uwanja wetu,” alisema.

Ameeleza kuwa kuwa ni muhimu kuhakikisha uwanja unakuwa na mazingira bora kwa ajili ya usalama wa wachezaji na ubora wa mchezo, akiongeza kuwa maboresho hayo ni sehemu ya mkakati wa kuinua michezo mkoani Tanga.

Aidha, amebainisha kuwa jitihada zinaendelea kuboresha nyasi za uwanja huo, huku mipango ya kuweka nyasi bandia ikiwa sehemu ya maboresho ya muda mrefu yatakayoongeza ubora na matumizi endelevu ya uwanja.

Rajab Abdalah ameongeza kuwa maboresho hayo pia yanalenga kukuza uchumi wa mkoa wa Tanga kwa kuvutia mashindano na timu mbalimbali zitakazokuja na mashabiki wao.

Kwa upande wake, Meneja wa Uwanja wa CCM Mkwakwani, Nasoro Makau, amesema kuwa utekelezaji wa kazi hiyo unaendelea vizuri na umefikia asilimia 40, akiahidi kuwa ndani ya muda mfupi kazi iliyobaki itakamilika.

“Kwa kasi hii tuliyonayo, tunaamini ndani ya muda mfupi tutakuwa tumemaliza kabisa ufungaji wa viti na uwanja kuwa tayari kwa matumizi kamili,” alisema meneja huyo.

Wadau wa klabu ya Coastal Union wamepongeza hatua hiyo wakieleza kuwa itakuwa suluhisho la changamoto ya muda mrefu ya kucheza nje ya mkoa.

Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Coastal Union, Abdalah Unenge, amesema maboresho hayo ni hatua kubwa kwa maendeleo ya timu hiyo na soka la Tanga kwa ujumla.

New Content Item (4)

“Haya ni maendeleo tunayoyasubiri kwa muda mrefu. Tukipata uwanja wa uhakika, tutarejesha nguvu ya timu yetu na ushindani utaongezeka,” alisema Unenge.

Naye Mwenyekiti wa matawi ya Coastal Union Mkoa wa Tanga, Salim Bawaziri, amesema kukamilika kwa uwanja huo kutaleta chachu mpya kwa mashabiki na wadau wa soka mkoani humo.

“Hii ni neema kwa Tanga. Tutakuwa na uwanja wa nyumbani nzuri wa kujivunia, mashabiki watarudi kwa wingi na timu yetu itapata sapoti kubwa zaidi,” alisema Bawaziri.

Maboresho ya Uwanja wa CCM Mkwakwani yanaendelea kuleta matumaini mapya kwa wadau wa michezo, huku yakitarajiwa kuinua kiwango cha soka na kuchochea uchumi wa mkoa wa Tanga.