Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Monduli wazindua mradi wa kuimarisha ulinzi wa mtoto

New Content Item (1)

Mkuu wa wilaya ya Monduli, Gloria Kimath akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa kuimarisha ulinzi wa mtoto. Picha na Bertha Ismail

Muktasari:

  • Mradi huo unatarajiwa kusaidia kuimarisha mifumo ya ulinzi wa mtoto na kupunguza changamoto za ukatili dhidi yao katika Wilaya ya Monduli na maeneo jirani.

Arusha. Halmashauri ya Wilaya ya Monduli imezindua utekelezaji wa Mradi wa “Arusha Standard Project” unaolenga kuimarisha ulinzi wa watoto, kusaidia familia zenye kipato duni na kutoa fursa endelevu za kuboresha maisha ya jamii katika wilaya hiyo.

Uzinduzi wa mradi huo umefanyika wakati taarifa za Wizara ya Maendeleo ya Jamii zinaonyesha kuwa changamoto kubwa za ukatili dhidi ya watoto nchini zinaendelea kugharimu ustawi wao.

Aidha takwim inaonyesha kuwa zaidi ya watoto 10,000 wanaoishi na kufanya kazi mitaani huokolewa Kila mwaka kutoka mazingira hatarishi wengi wakikimbia migogoro ya kifamilia na ukatili wa kijinsia.

Aidha, zaidi ya watoto 15,300 walio na umri chini ya miaka 18 wameripotiwa kufanyiwa ukatili wa kijinsia na manusura 19,717 Kwa mwaka 2025.

Mradi huo unaotekelezwa na Shirika lisilo la Kiserikali la SOS Children’s Villages unatarajiwa kufanyika kwa kipindi cha miaka mitatu, ukilenga kuwafikia watoto 2,000 pamoja na vijana 500 katika Wilaya ya Monduli.

Akizindua mradi huo, Mkuu wa Wilaya ya Monduli, Gloriana Kimath, amewataka wataalamu wa SOS pamoja na maofisa maendeleo ya jamii kushirikiana kwa karibu na viongozi wa kimila ili kurahisisha utekelezaji wa malengo ya mradi huo.

Amesema ushirikishwaji wa viongozi wa kimila ni nyenzo muhimu katika kufanikisha miradi ya maendeleo, hususan katika jamii zenye mifumo ya jadi kama ya Wilaya ya Monduli.

“Tunafahamu kwamba kila mtoto ana haki ya kulelewa katika familia yenye upendo, ulinzi na malezi bora, Hivyo mradi huu umekuja wakati muafaka katika kuunga mkono juhudi za Serikali kupitia programu jumuishi ya Taifa ya malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto"

"Lakini kumbukeni wilaya hii ina jamii kubwa ya Kimasai ambapo mila, tamaduni na desturi bado zina nafasi kubwa, hivyo mnaposhirikiana na wataalam wa maendeleo ya jamii msisahau wazee wa mila ambao wana sauti kubwa katika kaya na jamii kwa ujumla,” amesema Kimath.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa SOS Children’s Villages Tanzania, Thomas Kipingili, amesema mradi huo umejikita katika maeneo manne makuu, yakiwemo kutoa malezi mbadala kwa watoto walio katika mazingira hatarishi, kuwawezesha vijana kiuchumi na kijamii ili waweze kujitegemea, kuimarisha mahusiano ya kijamii na kupunguza umaskini.

New Content Item (1)

Mkurugenzi wa SOS Children’s Villages Tanzania, Thomas Kipingili akizungumzia utekelezaji wa mradi wa kuimarisha ulinzi wa mtoto katika wilaya ya Monduli

Amesema malengo mengine ni kuimarisha uwezo wa familia katika kutoa malezi bora na mifumo ya ulinzi wa watoto.

“Lengo letu ni kujenga jamii imara inayoweza kujitegemea, kwa kuwawezesha vijana kiuchumi na kuzipa familia uwezo wa kutoa malezi bora, na kuzuia kuvunjika kwa familia na kuimarisha ustawi wa watoto,” amesema Kipingili.

Naye Afisa Maendeleo ya Jamii wa Mkoa wa Arusha, Erena Materu, ameipongeza SOS Children’s Villages kwa kuanzisha mradi huo, akisema utasaidia kuongeza uelewa wa jamii kuhusu malezi na makuzi ya watoto, hususan wale wanaotoka katika mazingira magumu.

Mradi huo unatarajiwa kuwa na mchango mkubwa katika kuimarisha mifumo ya ulinzi wa mtoto na kupunguza changamoto za ukatili wa watoto katika Wilaya ya Monduli na maeneo jirani.