Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mradi wa maji kunufaisha wakazi elfu 21 Namungo

Tanki la maji linalojengwa na Kampuni ya Elianje katika eneo la Namungo  Kijiji cha Naunambe ambapo Tanki hilo  likikamilika litaweza kutoa lita za ujazo elfu 720.Picha na Bahati Mwatesa

Muktasari:

  • Katika hatua nyingine,Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa amezindua mradi wa barabara ya Mwilali  yenye urefu wa 0.59 kwa kiwango cha lami.

Ruangwa. Mradi wa maji Namungo utaondoa changamoto ya upatikanaji wa maji katika eneo hilo kwani shughuli zake za uchimbaji pamoja na uchenjuaji madini zinahitaji kiwango kikubwa cha maji ili kuongeza uzalishaji kwa ufanisi.

Akizungumza leo Ijumaa  Mei Mosi 2026 mbele ya mkimbiza mwenge wa uhuru Kitaifa, Wazo Mwang'onda, Ofisa Mahusiano Joseph Shayo, amesema kuwa mradi huo umegharimu Sh1 bilioni na ukimalizika utaweza kunufaisha wakazi elfu 21 katika eneo hilo la Namungo Kijiji cha Naunambe.

Ameendelea kusema kuwa kwasasa mahitaji ya maji kwa siku ni lita elfu 5 na mradi huo utakapokamilika mahitaji ya maji ni lita elfu 720 kwa siku.

"Kijiji hiki shughuri kubwa zinazofanyika ni uchimbaji wa madini na kazi zake zinatumia sana maji hivyo kuona kuwa kunauhitaji mkubwa wa maji Kampuni ya Elianje imeweza kutoa fedha kwaaajili ya kuchimba kisima cha maji kwaajili ya shughuliza migodi pamoja na wananchi wanaoishi kijijini hapo."amesema Shayo.

Mmoja wa wachimbaji wa madini kutoka Namungo Fahad Juma amesema kuwa mradi huo ukikamilika utakuwa umeondoa changamoto ya maji katika eneo hilo kwani wananchi watanufaika pamoja na wao wachimbaji na wachenjuaji wa madini watakwenda kufanya shughuli zao kwa urahisi.

"Tunashukuru Elianje kwa kuliona hili, kwani tutaweza kufanya shughuri zetu kwa ufanisi pamoja na wanachi watakuwa wameondokana na changamoto ya maji katika eneo hilo."amesema Juma.

Kwa upande wake mkimbiza mwenge wa uhuru Kitaifa, Mwangonda baada ya kuweka jiwe la msingi ameishukuru Kampuni ya Elianje kwa uwekezaji mkubwa katika eneo hilo kwani wananchi wanakwenda kuondokana na changamoto hiyo.

Kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru Kitaifa, Wazo Mwang'onda watatu kutoka kushoto  akiweka jiwe la msingi katika kijiji cha Naunambe .Picha na Bahati Mwatesa

"Niishukuru kampuni ya Elianje kwa uwekezaji huu mkubwa kwa kufanya wananchi kupata maji bure napia nikuombe Mkuu wa Wilaya wa Ruangwa kuweka mazingira rafiki kwa wawekezaji hawa."amesema Mwang'oka.

Katika hatua nyingine,Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa amezindua mradi wa barabara ya Mwilali  yenye urefu wa 0.59 kwa kiwango cha lami.

Kwa upande wake, Meneja wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (Tarura) Wilaya ya Ruangwa, Mashaka Nalupi, ameeleza kuwa katika mwaka wa fedha 2023/2024, Serikali kuu ilitoa Sh500milioni, kupitia Mfuko wa Barabara kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo.

Nalupi amesema kuwa lengo la mradi ni kuboresha miundombinu ya usafirishaji kwa wakazi wa vijiji vya Likangara, Dodoma, Nachingwea na Mchanganindani ndani ya Wilaya ya Ruangwa.