Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wakulima Pwani wapongeza ugawaji miche ya korosho, waeleza mabadiliko kiuchumi

Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakari Kunenge akigawa miche ya korosho Kwa wakulima. Picha na Sanjito Msafiri.

Muktasari:

  • Wakulima wa zao la korosho mkoani Pwani wamepongeza utaratibu wa ugawaji wa miche bora unaotekelezwa na Bodi ya Korosho Tanzania (CBT), wakisema umeambatana na elimu itakayoongeza uzalishaji na ubora wa zao hilo.

Kibaha. Wakulima wa zao la korosho mkoani Pwani wamepongeza utaratibu wa ugawaji wa miche bora ya korosho unaofanywa na Bodi ya Korosho Tanzania (CBT), wakisema mpango huo umezingatia uwazi na mahitaji halisi ya wakulima.

Shughuli ya ugawaji wa miche ya korosho imefanyika January 27, 2026 na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge huku akiwahimiza wakulima hao kuitumia kwa kufuata maelekezo kutoka kwa wataalamu wa kilimo ambao awali waliwaelekeza.

Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi leo Mkoani humo baadhi ya wakulima wa zao hilo wamesema utaratibu huo utawarahisishia kumudu gharama za kilimo ambazo awali zilikuwa zinawakabiri

“Ni jambo la faraja na matumaini kwakuwa kupara miche bora bila malipo itasaidia wakulima wengi kulima zao hilo kwa hamasa na kwa tija hivyo ni jambo la kushukuru tunaamini wengi watafikiwa na utaratibu huo,” amesema Ramadhani Mfinanga.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakari Kunenge akigawa miche ya korosho Kwa wakulima. Picha na Sanjito Msafiri.

Amesema kuwa awali walikuwa wanalima kwa mazoea, lakini sasa wameelekezwa kilimo cha kitaalamu. hivyo utaratibu huo ukidumishwa utaiwanua kiuchumi

Ester Yoweli amesema mpango wa ugawaji wa miche umeongeza matumaini mapya kwa wakulima wa mkoa wa Pwani, akieleza kuwa miche bora itapunguza gharama za uzalishaji na kuongeza mavuno.

“Hii ni fursa kubwa kwetu wakulima. Tunaiomba serikali iendelee na mpango huu ili kuwafikia wakulima wengi zaidi,” amesema Yoweli.

Bodi ya Korosho Tanzania (CBT) imegawa takribani miche 1,500,000 ya korosho kwa wakulima wa mkoa wa Pwani ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuongeza uzalishaji na ubora wa zao hilo nchini.

Akizungumza katika uzinduzi wa ugawaji wa miche hiyo uliofanyika Kijiji cha Chumbi “A”, Wilaya ya Rufiji, Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge amewahimiza wakulima kuzingatia miongozo bora ya upandaji ili kuzalisha korosho zenye viwango vinavyokubalika kwenye soko la kimataifa.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakari Kunenge akigawa miche ya korosho Kwa wakulima. Picha na Sanjito Msafiri.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa CBT Reuben Putaputa amesema miche iliyogawiwa ni sawa na asilimia 35.7 ya miche 4,200,000 iliyopangwa kusambazwa kwa wakulima wa korosho nchini, akieleza kuwa zoezi hilo limeanza mkoani Pwani na litaendelea katika mikoa mingine.

Zao la korosho lilianza kulimwa mkoani Pwani tangu kipindi cha ukoloni na limekuwa zao muhimu la biashara kwa wananchi wa wilaya za Rufiji, Kibiti na Mafia. Kwa miaka mingi, korosho limechangia kipato cha kaya, ajira na maendeleo ya jamii.

Maboresho ya miche, elimu ya kilimo bora na upatikanaji wa masoko yameendelea kulifanya zao hilo kuwa mhimili wa uchumi wa wakulima wa mkoa wa Pwani.