Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Watanzania Wanne kushuhudia mechi ya Mexico na England kupitia promosheni ya Mixx

Dar es Salaam. Watanzania wanne wamejishindia tiketi za safari ya kwenda Mexico kushuhudia mechi za Kombe la Dunia kupitia kampeni ya "Kila Muamala ni Bao la Ushindi", huku kampuni ya Mixx ikisema kampeni hiyo imeendelea kuongeza matumizi ya huduma za fedha kidijitali nchini.

Washindi hao ni Sumaiya Khamis wa Zanzibar, Deogratius Haule, Edwin Kambo na John Mzee. Washindi hao wataona mechi ‘live’ kati ya Mexico na England iliyopangwa kuchezwa Jumatatu, Julai 6, 2026.

Washindi hao, waliotoka katika mikoa mbalimbali ikiwemo Dar es Salaam, Zanzibar na Arusha, walikabidhiwa tiketi zao katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam na kuondoka Ijumaa, Julai 3,2026 kuelekea nchini Mexico.

Akizungumza katika hafla hiyo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Mixx, Angelica Pesha, alisema kampeni hiyo imeonyesha kuwa huduma za fedha kidijitali zinaweza kuwa zaidi ya njia ya kufanya miamala, kwa kuwa pia zinafungua fursa kwa wananchi.