Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala Tanzania limepiga marufuku matumizi na kuifutia usajili dawa ya Hensha maarufu mkongo inayomilikiwa na kituo cha Nyasosi Traditional Clinic cha jijini Dar es Salaam.

Hayo yamesemwa leo Jumatano Julai 27, 2022 mjini Morogoro na Mwenyekiti wa baraza hilo, Profesa Hamis Malepo wakati akizungumza na waandishi wa habari.