Mchungaji wa Kanisa la EAGT Kiloleli Mwanza, Dk Jacob Mutashi amesema hakuna jambo baya katika utumishi wa umma kama kiongozi wa umma kwenda Club (kumbi za starehe) na kukata mauno huku akisema viongozi wenye tabia hizo wanapaswa kuziacha.

 Dk Mutash ametoa kauli hiyo Ijumaa Oktoba 14, 2022 kwenye kongamano la kuenzi maisha ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere lililoandaliwa na kufanyika katika Chuo cha Mtakatifu Augustino (SAUT) Mwanza.