Mzee wa miaka 102 aliyepigana vita ya pili ya dunia asimulia maisha ya zamani, sasa
Muwakilishi wa Tanzania Legend, Mzee Omari Mhando Shangali (102) ambaye alipigana vita ya Pili ya Dunia amesema magonjwa yamekuwa mengi kipindi hiki kwa sababu ya matumizi ya mbolea kwenye kilimo.
Mzee Shangali ameyasema hayo leo Jumatatu Julai 25, 2022 wakati wa maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya mashujaa iliyofanyika viwanja vya mashujaa jijini Dodoma.