Rais Mwinyi ateua wakuu wa mikoa, wilaya

Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi

Muktasari:

  • Katika taarifa iliyotolewa leo Novemba 16, 2023 na Katibu Mkuu Kiongozi, Zena Said, Rais Mwinyi amemteua Ayoub Mohamed Mahmoud kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, kabla ya hapo Ayoub alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Unguja. Rais wa Zanzibar Dk Hussein Mwinyi amewateua wakuu wa Mikoa na Wilaya na wengine kuwabadilisha vituo vyao.

Katika taarifa iliyotolewa leo Novemba 16, 2023 na Katibu Mkuu Kiongozi, Zena Said, Rais Mwinyi amemteua Ayoub Mohamed Mahmoud kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, kabla ya hapo Ayoub alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Rashid Hadid Rashid ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja

Sadifa Juma Khamis aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini A, ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kati na nafasi yake kuchukuliwa na Othman Ali Maulid ambaye ni mstaafu wa utumishi wa umma.

Galos Nyimbo, mwanajeshi mstaafu ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya Kusini Unguja nafasi iliyokuwa inashikiliwa na Rajab Mkasaba.

Uteuzi huo unaanza leo na wateule wote wataapishaa Novemba 20, 2023 Ikulu Zanzibar.