Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rais Mwinyi awaapisha majaji wakiahidi kutenda haki, kuharakisha kesi

Muktasari:

  • Wamesema wnanchi wanapendelea haki zao zisicheleweshwe hivyo mbali na kusimamia hilo pia nao wamewasihi wananchi wasiogope kufika mahakamni kusaidia kutoa ushahidi kwa yale wanayoyafahamu.

Unguja. Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi amewaapisha majaji wawili kati ya watatu wa mahakama kuu aliowateua hivi karibuni wenyewe wakiahidi kusimamia, kuharakisha na kutenda haki katika chombo hicho cha kutafsiri sheria.

Jaji mteule ambaye hakuwepo katika kiapo hicho ni Raya Issa Msellem ambaye hata hivyo haikutolewa taarifa yoyote kuhusu kutokuwepo kwake.

Mbali na majaji hao pia Rais Mwinyi amewaapisha Mwenyekiti wa Tume ya Maadili ya viongozi wa Umma, Dk Mahadh Juma Maalim na Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Dk Josephine Kimaro.

Jaji Valentina Andrew Katema akila kiapo kuwa  Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar.

Wakizungumza na waandishi wa habari baada ya kuapishwa leo Julai 24, 2026 Ikulu Zanzibar, Majaji hao wamesema wanakwenda kusimamia na kutenda haki kwa mujibu wa sheria na miongozo ya kazi zao.

Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar, Valentine Andrew Katema amesema atahakikisha anaongozwa na busara na sheria kwa kutenda haki.

“Sitakwenda kinyume na utaratibu uliopo, kwa hiyo katika kufuata utaratibu, basi tutaweza kulinda haki zote za msingi,” amesema Jaji Katema.

Amesema jamii inapaswa kujua kwamba Mahakama ipo wazi na mtu yeyote mwenye tatizo kwenye upatikanaji wa haki, kwa maana ama ametendewa kosa na vyovyote vile, ni vyema kufuata taratibu za kisheria na kuhakikisha kwamba siku ya kesi anafika mahakamani.

Dk Mahadhi Juma Maalim akila kiapo kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma Zanzibar.

Ametumia fursa hiyo kuwasihi wananchi wasiogope kwenda mahakamani kutoa ushahidi ambao anaona unaweza kuleta tija katika uamuzi.

“Lakini hata inapofika kesi mahakamani, basi jamii iwe tayari kuisaidia mahakama kwenye kutoa ushahidi, kwamba wafike mahakamani watoe ushahidi ili hatimaye mahakama iweze kutoa uamuzi sahihi na wahaki,” amesema

Kwa mujibu wa Jaji Katema ambaye kabla ya nafasi hiyo alikuwa Mrajisi wa Mahakama, mwananchi asipofika mahakamani kutoa ushahidi, hatakuwa ameisaidia Mahakama katika kusimamia haki ambayo anaijua mhusika.

Lakini kwsababu lakini kwa sababu mahakama hujaweza kuisaidia, itatenda haki kwa mujibu wa kile ambacho kilichopo mahakamani.

Khamis Ali Simai akila kuapo kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar.

Jaji mwingine Khamis Ali Simai amesema wananchi wanapendelea zaidi haki zao zisicheleweshwe kwahiyo watajitahidi kwenda na kasi kesi zisikae mahakamani katika muda mwafaka lakini bila kuondoka kwenye misingi ya haki.

"Tutajitahidi, kama ilivyo Mahakama Kuu, kwamba kuweza kutoa haki kwa muda ambao mwafaka, bila kukaa sana mahakamani kesi, ili ziweze kumaliza kwa muda mwafaka.

“Nakwenda kusimamia kiapo namba tatu nilichoapa, kinaeleza kwamba nitafanya haki bila upendeleo, woga, chuki. Hivyo basi, tutaendelea na jitihada na kasi ya mahakama,” amesema

Amesema watahakikisha wanatekeleza haki hizo bila kuwa na muhali wa aina yoyote, kutekeleza majukumu ambayo kimsingi jamii imeweza kuwaamini kwa hilo.

Dk Josephine Kimaro akila kiapo kuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Zanzibar.

Naye Mwenyekiti wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Dk Mahadh Juma Maalim amesema hatua ya kwanza anakwenda kukutana na wadau wakubwa wa tume kwa ajili ya kuwasikiliza na kujifunza.

Kingine anachokwenda kufanya katika siku za kwanza ni kupitia nyaraka, kupitia maandishi mbalimbali, kwa ajili ya kuifahamu zaidi kazi ya tume na tume nyingine duniani zinazolingana na hii.

“Kwa hiyo, kwa siku za mwanzo, kazi yangu kubwa zaidi ni kujifunza, ili baadaye nije na mpango mzuri zaidi wa utekelezaji wa majukumu yangu,” amesema.