Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ushirika chachu ya maendeleo ya wananchi

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Kazi Uchumi na Uwekezaji, Shariff Ali Asharif akizungumza kuhusu siku ya ushirika inayotarajiwa kufanyika kesho Julai 5, 2025 Kizimkazi Mkao wa Kusini Unguja

Muktasari:

  • Siku ya ushirika duniani ilianzishwa mwaka 1923 na shirika la kimataifa linaloshughulikia vyama vya ushirika duniani.

Unguja. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi Uchumi na Uwekezaji, Shariff Ali Shariff amesema sekta ya ushirika Zanzibar ina mchango mkubwa katika kukuza maendeleo ya kijamii na kiuchumi, huku ikiwezesha wananchi kujikwamua na umasikini.

Ameeleza hayo Julai 4, 2025 akitoa taarifa ya maadhimisho ya Siku ya Ushirika Duniani inayotarajiwa kuadhimishwa kesho Julai 5, 2025. Maadhimisho yatafanyika Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja, mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi.

“Sekta ya ushirika imekuwa ni chombo madhubuti katika kuwawezesha wananchi, hasa wa kipato cha chini kushiriki kikamilifu katika shughuli za biashara na kiuchumi,” amesema.

Sekta ya ushirika Zanzibar amesema ina historia ndefu tangu miaka ya 1950 na baada ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya mwaka 1964, Serikali ilifanya jitihada ya kuviboresha na kuviwezesha vyama kufanya kazi kwa pamoja na kuleta tija kwao na Serikali kwa ujumla.

Waziri Shariff amesema Serikali kupitia Idara ya Ushirika imesajili vyama vya ushirika 779 vinavyojishughulisha na sekta mbalimbali zikiwamo za kilimo, uvuvi, ufugaji, huduma za kifedha (Saccos), viwanda vidogo na usarifu wa mazao.

Siku ya ushirika duniani ilianzishwa mwaka 1923 na shirika la kimataifa linaloshughulikia vyama vya ushirika duniani ambapo Umoja wa Mataifa uliitambua rasmi siku hii mwaka 1995 ikiwa ni ishara ya kutambua kazi  zinazofanywa na vyama hivyo katika kujikomboa kiuchumi, kupunguza umaskini na kuchochea maendeleo endelevu.

Siku hiyo huwakutanisha wanaushirika na wadau wa sekta ya ushirika nchini kwa kutoa nafasi ya kujifunza, kubadilishana uzoefu na kujadili kwa pamoja mafanikio, changamoto na kuzitafutia ufumbuzi.

Maadhimisho hayo hufanyika kila Jumamosi ya kwanza ya Julai. Kaulimbiu kwa mwaka huu ni: “Ushirika hujenga ulimwengu bora.”

Baadhi ya wananchi ambao wamejiunga kwenye ushirika, akiwamo Haji Said Ali amesema kuna faida nyingi kwani wamekuwa wakikopeshana kupitia Saccos ambayo ilianza kama vikoba.

“Mtu akiwa na shida anakopa au akitaka kufanya biashara anakopa kisha anarejesha kidogokidogo, mwanzoni unaweza kuona kama ni mchezo lakini kadri unavyokua unaona faida zake, unasaidia wengi,” amesema.