Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Washiriki 1,500 kushiriki jukwaa la kimataifa la teknolojia, AI kutoka Afrika

Waziri wa Mawasiliano, Teknolojia ya Habari na Ubunifu, Mudrik Ramadhan Soraga akizungumza na waandishi wa habari kuhusu jukwaa la kimataifa la Teknolojia na Akili Unde linalotarajiwa kufanyika Unguja, Zanzibar.

Muktasari:

  • Kuandaa tukio la kimataifa la teknolojia la kiwango hiki kunaiweka Zanzibar katika nafasi nzuri ya kuvutia uwekezaji unaotegemea teknolojia hususani katika maeneo ya Akili Unde, Teknolojia za kifedha (FinTech), Teknolojia za Kilimo (AgriTech) na utalii janja (smart Tourism).

Unguja. Wakati Jukwaa la Kimataifa la Teknolojia na Akili Unde (Tech an AI Internation Expo), likitarajiwa kufanyika Zanzibar, Serikali imesema inadhamiria kukifanya kisiwa hicho kuwa kitovu cha ubunifu na mageuzi ya kidijitali barani Afrika.

Jukwaa hilo ambalo limeandaliwa na Africa Business Inc ya Afrika Kusini kwa kushirikiana na Wizara ya Mawasiliano, Teknolojia ya Habari na Ubunifu na Kampuni ya The Unique Touch, linalenga kuwaleta pamoja watunga sera, wadau wa teknolojia kujadili na kuchochea ukuaji wa uchumi wa kidijitali.

Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari kuhusu jukwaa hilo Julai 24, 2026, Waziri wa Mawasiliano, Teknolojia ya Habari na Ubunifu, Mudrik Ramadhan Soraga amesema hatua hiyo ni kuiandaa Zanzibar kuvutia uwekezaji wa kampuni kubwa za kimtandao duniani.

"Tunataka kuona kampuni kubwa za teknolojia duniani kama Google, Amazon,Meta na nyinginezo zinaweka makao makuu yake hapa au matawi yake, na Zanzibar tuwe kitovu cha ubunifu. Ili kufikia huko ndio tunakuwa na majukwaa kama haya," amesema Soraga

Amesema Serikali inaendelea kuweka sera na mazingira rafiki kwa ajili ya uwekezaji na kuandaa sheria ambazo zinaendena na masuala ya teknolojia ili kuwa imara katika nyanja zote.

Mkurugenzi wa kampuni ya UT, Edwin George amesema wanalenga kukutanisha wataalamu kutoka mataifa mbalimbali katika nyanja tofauti.

Amesema AI imeanza kubadilisha mifumo ya kufanya biashara, kusoma hata katika uendeshaji wa serikali hivyo ni wakati muafaka kuelekea katika ulimwengu wa teknolojia.

"Ni muhimu kwa Zanzibar kuwa sehemu ya mabadiliko haya na kuhakikisha vijana wetu, wafanyabiashara, wabunifu na taasisi zetu zinapata nafasi kushiriki kikamilifu katika uchumi huu mpya wa kidijitali," amesema

Naye Mkurugenzi wa Ubunifu kutoka Wizara ya Mawasiliano, Tekenolojia ya Habari na Ubunifu, Samola John Chacha amesema kupitia jukwaa hilo Zanzibar itanufaika kwani itaongeza ujuzi na kutoa mwanga katika masula ya Tehama.

Akizungunza kwa njia ya mtandao, Ofisa Mkuu wa Masoko Africa Business Inc, Lebohang Norwana amesema jukwaa hilo ni muhimu.

Amesema nafasi ya kimkakati ya Zanzibar kijiografia pamoja na utajiri wake kiutamaduni na kihistoria inaifanya kuwa mahali muafaka pa kuandaa majukwaa makubwa ya kimataifa ya tekenolojia.

"Kwa muda mrefu Zanzibar imejulikana kwa fukwe zake za kuvutia na sekta yake ya utalii, lakini sasa inalenga kupanua uchumi wake kwa kutumia fursa zinazotokana na mapinduzi ya teknolojia ya kidijitali," amesema 

Kuandaa tukio la kimataifa la teknolojia la kiwango hiki kunaiweka Zanzibar katika nafasi nzuri ya kuvutia uwekezaji unaotegemea teknolojia hususani katika maeneo ya Akili Unde, Teknolojia za kifedha (FinTech), Teknolojia za Kilimo (AgriTech) na utalii janja (smart Tourism).

Jukwaa hilo linatarajiwa kufanyika kuanzia Septemba 24 hadi 26 Unguja Zanzibar na kuwakutanisha washiriki zaidi ya 1500 kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika.