Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ajali ya Hiace, lori yasababisha vifo vya watu watano

Muktasari:

Mkuu wa Wilaya ya Muleba amesema miongoni mwa waliokufa ni dereva wa Hiace na kondakta.

 Muleba. Watu watano wamefariki dunia baada ya gari aina ya Toyota Hiace kugongana na lori kisha kuwaka moto.

Ajali hiyo imetokea katika Kijiji cha Kyamyorwa wilayani Muleba mkoani Kagera.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Augustino Olomi amesema ajali hiyo imetokea leo Ijumaa Oktoba 20, saa 12:00 asubuhi.

Amesema mwendo kasi wa dereva wa gari dogo la abiria ni chanzo cha ajali hiyo.

Ingawa Kamanda Olomi hakuwataja waliokufa, Mkuu wa Wilaya ya Muleba, Richard Ruyango amesema miongoni mwao ni dereva wa gari dogo, kondakta na abiria watatu.

Amesema watu hao walishindwa kujiokoa kutokana na mlango wa gari kubanwa hivyo kushindwa kufunguka.