Kivuko cha Mv Nyerere hiki hapa

Kivuko cha Mv. Nyerere kikiwa kimegeuzwa na kusimama wima leo mchana. Picha na Jovither Kaijage

Muktasari:

  • Kivuko cha Mv Nyerere kilichopinduka Alhamisi Septemba 20, 2018 hatua chache kutoka gati la kijiji cha Bwisya kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe kimenyanyuliwa baada ya jitihada za siku tano za wataalam wa uokoaji kutoka JWTZ na vikosi mbalimbali


Ukara.  Hatimaye kivuko cha Mv Nyerere kilichopinduka Alhamisi Septemba 20, 2018 kimenyanyuliwa leo mchana Alhamisi Septemba 27, 2018.

Kivuko hicho kimenyanyuliwa baada ya jitihada za siku tano tangu Jumapili Septemba 23, 2018 zilizofanywa na wataalam wa uokoaji kutoka vyombo vya ulinzi na usalama wakiongozwa na maofisa wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).

Wataalam hao walikuwa wakifanya kazi ya kukinyanyua kivuko hicho usiku na mchana huku wakitumia njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupitisha maboya chini ya maji, kuyajaza upepo sambamba na kukifunga kamba kivuko hicho na kukivuta.

 

Soma Zaidi: