Juhudi za kukinyanyua kivuko cha Mv Nyerere zaanza kuonekana

Jitihada za kukinyanyua kivuko cha Mv Nyerere zinaanza kutia matumaini baada wataalam wa uokoaji kufanikiwa kupitisha maboya chini ya maji  na sasa sehemu kubwa ya kivuko hicho inaonekana. Picha na Peter Saramba

Muktasari:

  • Kazi ya kukinyanyua na kukigeuza kivuko cha Mv Nyerere inayoendelea katika ufukwe wa kijiji cha Bwisya kisiwa cha Ukara imeanza kuzaa matunda baada ya sehemu kubwa ya kivuko hicho kuibuliwa kutoka ndani ya maji


Ukara. Jitihada za wataalam wa uokoaji kukinyanyua na kukigeuza kivuko cha Mv Nyerere zimeanza kuonyesha matumaini baada ya sehemu kubwa kivuko hicho kupandishwa juu ya maji.

Mafanikio haya yanatokana na kazi iliyoanza kufanywa jana Jumatano Septemba 26, 2018 na wataalam hao kupitisha maboya maalum chini ya maji yaliyofanikisha kukisukuma juu.

Pamoja na maboya hayo, wataalam hao pia wametumia mbinu ya kujaza maji ndani ya meli ya Mv Nyakibalya na kuyapunguza kidogo kidogo huku Mv Nyerere iliyofungwa kwa kamba kwenye meli hiyo nayo ikipanda juu ya maji.

Karibia ubavu wote wa kushoto wa kivuko cha Mv Nyerere ipo juu ya maji ikionekana kwa macho tofauti na ilivyokuwa awali ambapo kilikuwa ndani ya maji.

Kivuko cha Mv Nyerere kilipinduka Septemba 20, 2018 na hadi sasa watu 230 wamekufa na miili yao kuopolewa. Watu 41 walinusurika katika ajali hiyo.

Soma zaidi: