Lissu atoka ICU aona jua kwa mara ya kwanza tangu apigwe risasi

Muktasari:

  • Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumanne, Mbowe amesema afya ya Lissu inaimarika kwa kuwa alihitaji upasuaji mwingi sana kutokana na risasi zilizoingia kwenye mwili wake.

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema kuwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu ametoka ICU na sasa anaweza kukaa.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumanne, Mbowe amesema afya ya Lissu inaimarika kwa kuwa alihitaji upasuaji mwingi sana kutokana na risasi zilizoingia kwenye mwili wake.

“Amefanyiwa upasuaji mkubwa mara 17 mpaka sasa. Ameongezewa damu nyingi kuliko mtu yeyote miaka 20 iliyopita ametoka ICU wiki iliyopita,” amesema Mbowe.

Amesema Lissu hatumii oxygen tena wala mirija na kwamba anakula chakula anachokitaka.

“Juzi kwa mara ya kwanza alikaa, anatembea Wheel Chair na aliliona jua kwa mara ya kwanza,” amesema Mbowe.

“Tunawashukuru madaktari wa Dodoma na Nairobi. Hospitali ya Nairobi imefikisha awamu ya pili ya kutibu. Tunavyozungumza baada ya wiki moja kadri madaktari watakavyoshauri atamaliza matibabu ya pili,”

“Ataanza awamu ya tatu nje ya Nairobi yatakayokuwa ya muda mrefu. Kwa usalama wake hatutataja wapi anakwenda. Siyo Tanzania na sio jirani. Hiyo ndio hali halisi ya mgonjwa.”