Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Profesa JKCI aeleza walivyochunguza moyo wa Manji

Mfanyabiashara Yusuf Manji.

Muktasari:

Mfanyabiashara Yusuf Manji, ameanza kujitetea baada ya upande wa mashtaka kufunga ushahidi ulitolewa na mashahidi watatu.

Dar es Salaam. Daktari katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu namna walivyouchunguza moyo wa mfanyabiashara Yusuf Manji.   

Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Profesa  Mohammed Janabi (51) ametoa ushahidi wa upande wa utetezi katika kesi ya kutumia dawa za kulevya inayomkabili Manji.

Profesa Janabi ameieleza Mahakama jinsi walivyoangalia vyuma vilivyopo kwenye moyo wa Manji kama vimeziba au la.

Akiwa shahidi wa kwanza wa upande wa utetezi, Profesa Janabi aliongozwa na wakili Hajra Mungula kutoa ushahidi mbele ya Hakimu Mfawidhi, Cyprian Mkeha.

Manji ambaye katika hati ya mashtaka jina lake ni Yusufali Manji, alifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Februari 16 akidaiwa kati ya Februari 6 na 9 katika eneo la Sea View, Upanga wilayani Ilala alitumia dawa za kulevya aina ya Heroin.