Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rais Zuma ataka Ziwa Victoria libadilishwe jina

Muktasari:

·Ziwa Victoria ambalo linasifika kwa samaki linatumiwa pia na nchi za Tanzania na Kenya.

Dar es Salaam. Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma ameitaka Uganda kubadili jina la Ziwa Victoria ili liendane na jina linalowakilisha uhalisia wa wananchi wa eneo hilo.


Kiongozi huyo anayekosolewa vikali nchini mwake amesema tayari amemfahamisha Rais Yoweri Museveni juu ya haja ya kubadilishwa jina hilo.


Jina la Ziwa Victoria lilitolewa na mtafiti mmoja wa Uingereza kama zawadi kwa Malkia wa Taifa hilo aliyetambulika kwa jina la Victoria.


Akizungumza katika ufunguzi wa maonyesho ya utalii mjini Kampala, Rais Zuma amesema  Ziwa hilo kuendelea kuitwa  Victoria kunawanyima fursa wananchi wa eneo hilo kujivunia uasili wao.


 “Mnaweza kuweka bango kubwa linaloonyesha jina la jipya na kisha mkaweka bango  dogo litakalosomeka kama “ zamani eneo hili liliitwa Ziwa Victoria”. Lazima mbadilishe jina hili na kuweka jina litakaloelezea uzuri wa Taifa hili,” amesema Rais Zuma.