Mikel Arteta amshukia Mesut Ozil

Friday October 23 2020
ozil pic

London, England. Mikel Arteta amejibu tuhuma za Mesut Ozil kuwa ameshindwa kumheshimu akimjibu kiungo huyo kuwa ajilaumu mwenyewe kwania lishindwa kutimiza majukumu yake.

Kocha huyo wa Arsenal alimjibu Ozil kuwa ameleta vita ndani ya klabu ambayo haina ukweli kwa kuwatumuhu benchi la ufundi kwa kukosa shima na kuona thamani yake.

Ozil alitoa taarifa ya kuachwa kwake katika mtandao wa kijamii baada ya kuvuja kwa taarifa kuwa Arsenal imemtoa katika orodha ya wachezaji watakaiwakilisha klabu hiyo kwenye Ligi Kuu England.

Lakini Arteta alisisitiza kuwa Ozil hana mtu wa kumlaumu zaidi ya yeye mwenyewe, akimaanisha kuwa nyota huyo wa kimataifa wa Ujerumani alishacheza mechi ya mwisho ya klabu hiyo.

Kocha huyo raia wa Hispania alisema: “Kitu kinachotokea kwa Ozil kwa sasa si kitu kipya.

“Hali niliyomkuta nayo wakati najiunga na klabu hii ilikuwa ngumu, mambo haya yamekuwa yakitokea kwa miaka nane sasa.

Advertisement

“Kazi yangu ni kuimarisha viwango vya wachezaji kuleta timu bora uwanjani, lakini kwa sasa nahisi kama nimefeli.

“Nilitaka Mesut mwenye kiwango bora na wakati tukimaliza mchakato, sikuwa na uwezo wa kumaliza hilo kwa ubora kwasababu nilitakiwa kufanya uamuzi na kumwacha nje ya kikosi.

“Hilo halihusiani na tabia ya mtu wala suala la mshahara kama ambavyo nimekuwa nikisoma katika mitandao. Hilo halina ukwelo wowote.

“Nimeajiriwa kama kocha kwa ajili ya kushinda mechi za klabu hii na natakiwa kufanya uamuzi kupata timu bora kutoka katika timu hii.”

Advertisement