Pogba bado iweka roho juu Manchester United

Tuesday August 13 2019

 

Paul Pogba ameiweka njiapanda Manchester United kuhusu usajili wake wa majira ya kiangazi.

Licha ya kucheza kwa kiwango bora katika mchezo wa ufunguzi wa Ligi Kuu England walioshinda mabao 4-0 dhidi ya Chelsea, Pogba hajatulia.

Pogba alisema muda ukifika utaamua atakuwa klabu gani, kauli ambayo inaonyesha bado ana dhamira ya kuondoka Old Trafford.

Real Madrid imekuwa ikimuwinda mchezaji huyo wa Ufaransa katika usajili wa majira ya kiangazi.

Advertisement