Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Lampard amtambia Klopp kisa Kante karudi kikosini Chelsea

London, England. Kocha Frank Lampard amewaambia Liverpool wanaoonolewa na Jurgen Klopp wasiende kichwa kichwa Stamford Bridge kwa sababu viungo wake wawili N’Golo Kante na Mason Mount wote wamepona na wapo fiti kukipiga kwenye kipute hicho cha Ligi Kuu England.
Liverpool watawafuata The Blues huko Stamford Bridge leo Jumapili kwenye mchezo wa Ligi Kuu England na awali kocha Lampard alikuwa na wasiwasi wa kuwakosa mastaa wake hao muhimu, lakini sasa amedai, wanaweza kuwapo uwanjani kukipiga.
Mount amekuwa kwenye kiwango bora kabisa akiwa amefunga mabao matatu msimu huu, kitu ambacho kinamfanya Lampard kufurahia zaidi kama atakuwapo uwanjani kuwakabili vinara Liverpool, ambao hawajafunga mechi yoyote kwenye ligi hadi sasa.
Kurudi kwa Kante pia kunamfanya Lampard kujiamini zaidi kwa sababu anafahamu umuhimu wa mchezaji huyo kwenye kiungo katika kuwadhibiti Liverpool wasifanya maangamizi zaidi. Lampard alisema Kante ameanza mazoezi na atamfikiria kumpanga kwenye mchezo huo.
“Hii inasaidia sana, tunafahamu umuhimu wake. Kitu pekee cha kujiuliza kwa sasa yupo fiti kwa kiasi gani,” alisema.
“Amecheza mechi kadhaa, lakini hakucheza zile za kujiandaa na msimu mpya. Tunatazama, kama atakuwa kwenye hali nzuri tunayoitaka, tutamchezesha.”
Mechi nyingine za Ligi Kuu England zitakazopigwa leo Jumapili, Crystal Palace na supastaa wa Wilfried Zaha watakuwa nyumbani Selhurst Park kuw akaribisha Wol ves, wakati West Ham United watakuwa huko London kukipiga na jeshi la Ole Gunnar Solskjaer, Manchester United na Arsenal watajimwaga uwanjani kwao Emirates kukipiga na Aston Villa.