Mimi Mars kuwania tuzo za filamu Kenya

Wednesday November 6 2019

 

By Nasra Abdallah, Mwananchi [email protected]

Dar es Salaam. Msanii wa Bongo Fleva nchini Tanzania, Mimi Mars ametajwa kuwania tuzo za filamu nchini Kenya zijulikanazo kama Kalasha Awards.

Mimi Mars ni mdogo wa msanii mwingine wa Tanzania,  Vanessa Mdee.

Mimi Mars ambaye jina lake halisi ni Marian Mdee ametajwa  na bodi ya filamu ya nchini Kenya inayoandaa tuzo hizo.

Msanii huyo anawania kipengele cha msanii bora wa kike kupitia filamu ya ‘You Again’ iliyozinduliwa Septemba, 2019 nchini Kenya.

Mimi Mars anayetamba na nyimbo za Shuga, Sitamani, Mua, Kodoo na Papara atachuana na wasanii Mourine Obare, Sarah Hassan, Victoria Gadiora na Mwajuma Belle.

Upigaji kura kwa washindi umeanza tangu Oktoba 30, 2019 na mwisho ni Novemba 31, 2019.

Advertisement

Advertisement