Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ghasia ajiuzulu uenyekiti kamati ya Bunge ya Bajeti

Muktasari:

Taarifa ya kujiuzulu kwa Ghasia katika kamati hiyo imethibitishwa na Katibu wa Bunge

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Hawa Ghasia na makamu mwenyekiti wa kamati hiyo, Jitu Soni wamejiuzulu nafasi hizo, MCL Digital imeelezwa leo Jumanne Agosti 28, 2018.

Ghasia ambaye ni mbunge wa Mtwara Vijijini (CCM) na Soni (Babati Vijijini), wametangaza uamuzi wao huo leo asubuhi mjini Dodoma mbele ya wajumbe wa kamati hiyo.

MCL Digital imezungumza na Katibu wa Bunge, Stephen Kagaigai kuhusu kujiuzulu kwa viongozi hao na kubainisha kuwa ni kweli wamejiuzulu.

"Ni kweli wamejiuzulu nafasi zao na mimi sijajua kwa nini wamejiuzulu,” amesema.

Kwa taarifa zaidi endelea kufuatilia mitandao ya Mwananchi.