Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

JPM aeleza faida uanzishwaji kwa viwanda kila mkoa

Muktasari:

Ametoa kauli hiyo wakati akizindua kiwanda cha sigara cha Philip Moris


Morogoro. Rais John Magufuli amesema uazishwaji wa viwanda katika kila mkoa utasaidia kuondoa kero zilizokuwa zikilalamikiwa wakulima wa tumbaku hasa Mkoa wa Tabora. 

Akizungumza leo Machi 15, 2018 katika uzinduzi wa kiwanda cha sigara cha Philip Moris mjini Morogoro, Rais Magufuli amewataka Watanzania kubadilika kwa kuwekeza katika viwanda, kwamba suala la viwanda linawezekana na enzi za Morogoro ya viwanda itawezekana.

“Tusirudie tena kuua viwanda Serikali itaunga mkono viwanda vyote vinavyoanzishwa. Nafahamu kuna baadhi ya vikodi kodi vinavyoleta kero, tayari nimeshatoa maelekezo kwa waziri wa viwanda kuangalia upya hizo kodi,” amesema. 

“Wawekezaji tutalinda viwanda msihofu kujenga viwanda. Niwaombe viongozi wenzangu tusiwe vikwazo kwa wawekezaji kuja kuwekeza.”