Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

VIDEO: Maisha mapya ya wafanyakazi Clouds bila Ruge

Muktasari:

Wasema marehemu aliwatengeneza kina Ruge wengi wanaamini baada ya muda watakaa sawa


Dar es Salaam. Ingawa sio wote walioripoti ofisini baada ya kumaliza mazishi siku tatu zilizopita, wachache wameendelea na kazi kama ilivyoshuhudiwa na waandishi wa MCL Digital.

Shaffih Dauda ambaye ni mkurugenzi wa vipindi wa Redio Clouds anasema  wanaumia lakini wanaweza kuendelea na maisha kwa kuenzi matendo yake aliyokuwa  akipenda yafanyike enzi za uhai wake.

Amesema Ruge hakuwa mchoyo wa maarifa kitu ambacho kimefanya kampuni yao iwe na jeshi kubwa litakaloendeleza aliyopenda.

Naye mtangazaji, Kennedy the Remedy amesema bosi wao amewaachia utajiri mkubwa wa maarifa mfano wa mtu aliyekuwa akiwaandaa kuwa warithi wake atakapoondoka.

“Kama unavyoona bado hatujakaa vizuri lakini kusema ukweli tupo tayari kumuenzi bosi wetu kwa kupiga kazi na kujiamini kama alivyopenda kila mmoja wetu afanye,” amesema Kennedy.