Majina 73 ya wakurugenzi yaliyotajwa mahakamani kuwa makada wa CCM

Dar es Salaam. Mei 10 mwaka huu, Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ilitoa uamuzi na kuwaengua wakurugenzi wa halmashauri za majiji, miji/wilaya na manispaa kusimamia chaguzi mbalimbali nchini.

Wakurugenzi hao ambao wamekuwa wakilalamikiwa na vyama vya upinzani kuwa baadhi yao ni makada wa Chama cha Mapinduzi (CCM), ndio wasimamizi wa uchaguzi kwa mujibu wa Sheria ya Taifa ya Uchaguzi kifungu cha 7(1).

Lakini, Mahakama Kuu katika hukumu yake pamoja na mambo mengine ilibatilisha kifungu hicho ikieleza kuwa kinakinzana na Katiba ya nchi Ibara za 21(1), (2) na ya 26(1), kuhusiana na ushiriki katika shughuli za uchaguzi na kutii na kufuata Katiba na sheria.

Hukumu hiyo ilitolewa na jopo la majaji watatu; Dk Atuganile Ngala (kiongozi wa jopo), Dk Benhajj Masoud na Firmin Matogolo kufuatia kesi ya kikatiba namba 17, ya mwaka 2018 iliyofunguliwa mahakamani hapo.

Kesi hiyo ilifunguliwa na watetezi na wanaharakati wa haki za binadamu na demokrasia kwa kushirikiana na vyama vya siasa, kupitia kwa mwanaharakati Bob Wangwe dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Mkurugenzi wa Uchaguzi.

Pamoja na mambo mengine, Wangwe ambaye pia ni mkurugenzi wa Jukwaa la Katiba alikuwa akidai kuwa wakurugenzi hao ni wateule wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye kwa sasa ndiye mwenyekiti wa CCM, chama ambacho pia hushiriki katika uchaguzi.

Alikuwa anadai kuwa hiyo ni kinyume cha Ibara ya 74 (14 ) ya Katiba ya nchi ambayo inapiga marufuku kwa mtu yeyote anayehusika na uchaguzi kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa na kwamba ana haki ya kupiga kura tu.

Katika kuweka uzito madai yake, Wangwe aliyekuwa akiwakilishwa na Wakili Fatma Karume aliwasilisha mahakamani hapo orodha ya majina ya wakurugenzi 73 na ushahidi kuwa ama ni makada wa CCM au waliwahi kushiriki katika kugombea au kuomba kugombea nafasi mbalimbali kupitia chama hicho.

Wakati ikitoa uamuzi wake Mahakama ilisema kuwa imeridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo kuwa orodha ya majina ya wakurugenzi hao ni wanachama wa CCM kwa kuwa Serikali ilishindwa kuthibitisha kuwa si wanachama wa CCM.

Mahakama hiyo ilisema kuwa jambo hilo linaweza kuathiri utendaj kazi wao wa uhuru na haki kutokana na kuwa na maslahi na chama hicho, kinyume cha matakwa ya katiba ambayo inataka tume hiyo iwe huru katika kutekeleza majukumu yake.

Majina hayo ambayo Mwananchi imeyaona yamechapishwa pembeni kulia mwa habari hii.

Katika kutilia uzito madai yake kama kielelezo cha ushahidi wa madai yake, Wangwe aliwasilisha mahakamani orodha ya majina ya wakurugenzi aliodai ni miongoni mwa makada wa CCM.

Katika orodha hiyo alibainisha pia na vituo vyao vya kazi kwa sasa, nafasi walizowahi kuomba kuteuliwa (kura za maoni) katika uchaguzi mkuu hasa mwaka 2015, nafasi walizowahi kuziomba au walizokuwa wakizishikilia ndani ya chama na itikadi zao.

Naibu Waziri atetea

Akizungumzia wakurugenzi hao kutajwa kushiriki katika chaguzi, naibu waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Josephat Kandege alisema Rais John Magufuli huteua wakurugenzi kwa kigezo cha uwezo na siyo ukada wa CCM, alisema bila kuhusisha kesi iliyopo mahakamani.

Alisema wapo makada wengi ‘kindakindaki’ hawakuteuliwa kwa kigezo hicho, na baadhi waliteuliwa kisha wakaondolewa katika nafasi hizo baada ya kushindwa kufanya vizuri, akisema Rais hufanya uteuzi akihitaji kiongozi wa kumsaidia katika kusukuma maendeleo.

Waziri Kandege alipotakiwa kutoa ufafanuzi wa uteuzi wa makada wa CCM katika nafasi ya ukurugenzi, ambao kisheria ni watumishi wa umma wasiotakiwa kuathiriwa na itikadi za vyama alisema, “hakuna hata siku moja (mkurugenzi) atasimama jukwaani aseme CCM oyee, kumbuka kuna watu wanateuliwa na wasipo-perform wanaondolewa, kwa hiyo kinachombeba si ukada ni sifa ya utendaji wake, huwezi kubebwa na ukada wa kindakindaki, mbona wako wengi? Wangekuwa wamebebwa sana.

Alipoulizwa ni kwa nini Rais amekuwa akiteua makada kuongoza nafasi hizo wakati inaweza kuathiri uhuru wao katika kuwatumikia wananchi wote bila kujali itikadi, Kandege alisema, “Katika hali ya kawaida hivi utajua mchezaji fulani anafaa kuchezea Simba kama hujawahi kumwona akicheza?”

Alisema miongoni mwa wateule hao wa Rais wengi huwa na taaluma zao licha ya kuwa ndani ya chama, akifafanua mchakato wa kumpata mkurugenzi ni mkubwa.

Kuhusu hoja ya uhalali wa wakurugenzi kusimamia au kutosimamia chaguzi wakati ni makada wa CCM, Kandege alisita kuzungumzia suala hilo akidai ni kuingilia muhimili wa mahakama.

Wakati wa usikilizwaji wa kesi hiyo, Wangwe kupitia kwa Wakili wake Karume aliwasilisha picha mbalimbali za wakurugenzi hao na wasimamizi wengine aliodai kuwa waliteuliwa na NEC wakiwa wamevaa sare za CCM.

MAJINA YA WAKURUGENZI YALIYOPELEKWA MAHAKAMANIJina la mkurugenzi Kituo cha kazi Kura za maoni

 

1. Dk Wilson Mahera Charles Manispaa Arusha 2012

 

2.Banda Kamwende Sonoko Karatu urais 2015

 

,3. Stephen Anderson Ulaya Monduli DC Mtera 2015,

 

4. Juma Mhina Longido Kawe 2015 5. Stephen Edward Katembe Kigamboni Kyelwa 2015

 

6.Kayombo Lipes John Ubungo MNEC- vyuoni

 

7. Aron Kagumjuli Kinondoni Kada

 

 8. Kibasa Falesy Mohamed Kondoa Iringa mjini 2015

 

9. Khalifa Kondo Mponda Kondoa Mji Moro Mash-Kus 2015

 

10. Athuman Hamis Masasi Chamwino Manyoni Mash-201

 

11. Aloyce Kwezi Kilolo Kaliua 2015

 

12. Dk. Riziki Shemdoe Mufindi Lushoto 2015

 

13. Abdulaaziz Jaad Hussein Bukoba Kada

 

14. Gowin Moses Kitonka Karagwe Kahama 2015

 

15. Ngalinda Hawamu Ahmada Mpanda Kyerwa 201516. Michael Francis Nzyungu Mpanda Manisp. Kada

 

17. Joachim Jimmy Nchunda Nsimbo Ngara 2015

 

18. Anosta Lazaro Nyamoga Buhigwe Kilolo 201519. Lusubilo Joel Mwakabibi Kankoko Kada

 

20. Godfrey Msongwe Masekenya Kasulu Ileje 201521. Yohana Elia Sintoo Hai Singida Kask 2015

 

22. Shija Ana Clare Same Sengerema 201523. Golden A. Mgonzo Mwanga Mufindi Kus 2015

 

24. Justine Joseph Monko Liwale Singida Kask 201525. Bakari Mohamed Bakari Nachingwea Mkinga 2015

 

26. Yefred Edson Myezi Simanjiro Kilolo 2015

 

27. Tamim Kambona Kiteto Kada

 

28. Hamis Iddi Malinga Babati Ismani 201529. Amosi Jeremia Kusaja Bunda CCM 2012

 

30. Janeth Peter Mayanja Bunda Mji Mtama 2015

 

31. Hidaya Adam Usanga Tarime Mji Malinyi 2015, ACT

 

32. Mussa Joseph Mgata Kyela Njombe Kask 2015

 

33. Kivuma Hamis Msangi Mbarali Mbagala 2015

 

34. Elias Philemon Nawela Songwe Kawe 201535. Francis Kumba Ndulane Ifakara Kilwa Kask 2015

 

36. Florent Laurent Kayombo Mvomero Nkenge 2015

 

37. Audax Christian Rukonge Ulanga Kragwe 2015

 

38. Marcelin Rafael Ndimbwa Malinyi Ileje 201539. Omar Juma Kipanga Mtwara Kada, 2012