VIDEO: Taharuki bungeni, wabunge watimua mbio

Muktasari:

Hali hiyo imetokea baada ya mitambo ya tahadhari ya Bunge kulia kwa dakika tano.


Dodoma. Mwenyekiti wa Bunge, Najma Giga leo Februari 5, 2019 amelazimika kusitisha kikao cha Bunge baada ya mlio wa tahadhari bungeni kulia kwa muda mrefu.

"Naomba kusitisha Bunge kwa muda," amesema huku baadhi ya Bunge wakitoka huku wengine wakikimbia kutoka ukumbini kupitia milango ya dharura.

Mitambo ya tahadhari (alarm) hiyo ilianza kupiga saa 5:02 hadi saa 5:08 asubuhi na kuanza kulia tena baada ya dakika kama 10.

Alamu hiyo ilianza kulia saa 5:02 hadi saa 5:08 asubuhi  na kuanza kulia tena baada ya dakika kama 10 hivi.

Miongoni mwa waliotoka ndani ni Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto amefika bungeni na kusema ni mapema kutaja chanzo cha kulia kwa alamu hiyo lakini vyombo vya usalama ikiwamo Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji wanashughulikia kujua tatizo nini.

 

Endelea kufuatilia kujua kinachojiri bungeni