Waziri aeleza wizi ukarabati reli Tanga-Kilimanjaro

Muktasari:

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,  Atashasta Nditiye amesema mataluma ya reli 960  yaliibiwa wakati wa ukarabati wa reli kutoka Tanga hadi mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro


Moshi. Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,  Atashasta Nditiye amesema mataluma ya reli 960  yaliibiwa wakati wa ukarabati wa reli kutoka Tanga hadi mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro.

Ametoa kauli hiyo leo Jumamosi Julai 20, 2019 katika hafla ya uzinduzi wa safari mpya ya treni ya mizigo kuanzia Dar es Salaam-Tanga hadi Kilimanjaro ambayo kwa zaidi ya miaka 12 ilikuwa haitumiki.

Katika uzinduzi huo uliofanywa na Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa, naibu waziri huyo amesema, “Katika utengenezaji wa kipande cha urefu wa kilomita sita ilitokea hujuma ikiwa ni pamoja na vipande hivyo vya reli kuibwa.”

Amesema hali hiyo imeigharimu Serikali zaidi ya Sh2.2 bilioni,”

"Nawaomba Watanzania tulinde miundo mbinu ya reli zetu, TRC (Shirika la Reli Tanzania) wekeni  alama kwenye maeneo yote ya reli yenye vivuko ili kuepuka ajali zinazoweza kuepukika pamoja na kutoa  elimu kwa wananchi.”