Roboti la kufanya kazi za ujenzi laanza kuuzwa

Kukua kwa teknolojia kunakuja na mambo mengi, ikiwamo urahisishaji wa kazi.

Teknolojia imeiwezesha kampuni ya Boston Dynamics kutengeneza roboti ghali iitwayo Spot.

Roboti hiyo imetengenezwa kusaidia katika sekta za ujenzi, uchimbaji madini. Kwa namna alivyotengenezwa roboti huyo anaweza kuongezewa uwezo wa kufanya kazi nyingi zaidi ikiwamo kubeba mizigo mingi na kufika sehemu ngumu kwa binadamu kufika na kuchora ramani maalumu kwa ujenzi kulingana na alivyoelekezwa.

Kabla hujafikiria kuwa naye fikiria bei kwanza, roboti huyo anauzwa dola 37,000 za ambazo zinakaribia Sh85 milioni za Tanzania.