Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbunge mwingine wa upinzani ajiunga CCM leo

Muktasari:

  • Ametangaza uamuzi huo leo katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika katika ofisi ndogo za CCM Lumumba jijini hapa, akiwa sambamba na Katibu Mkuu wa chama hicho tawala, Dk Bashiru Ally.

Dar es Salaam. Mbunge wa Liwale kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF), Zuberi Kuchauka leo Jumatatu Agosti 13, 2018 ametangaza kujiunga na CCM.

Ametangaza uamuzi huo leo katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika katika ofisi ndogo za CCM Lumumba jijini hapa, akiwa sambamba na Katibu Mkuu wa chama hicho tawala, Dk Bashiru Ally.

Kuchauka amesema moja ya sababu iliyomuondoa CUF ni utendaji kazi wa Rais John Magufuli pamoja na mgogoro unaokitafuta CUF.

CUF imekumbwa na mgogoro tangu Profesa Ibrahim Lipumba kurejea katika uongozi mwaka 2016, ikiwa ni mwaka mmoja tangu alipojiuzulu uenyekiti wa chama hicho.