Pwani, Manyara zaanza kwa kishindo michuano ya Umitashumta

Monday June 19 2017

 

By Saddam Sadick,mwananchi [email protected]

Timu za Mikoa ya Pwani na Manyara zimeanza vyema mashindano ya Umoja wa Michezo kwa Shule za Msingi Tanzania (Umitashumta) kwa kuzichapa Rukwa na Kigoma kwenye viwanja vya Chuo cha Ualimu Butimba jijini Dar es Salaam.

Katika michezo ya ufunguzi, Pwani iliinyuka Rukwa kwa bao 1-0 katika mchezo wa soka kwa wavulana, huku Manyara walinyamazisha Kigoma katika mchezo wa Wavu kwa Wavulana kwa seti 3-0.

Katika soka, Pwani ilibidi kusubili hadi dakika 87, wakati mchezaji wake Mahamoud Mbonde alipofunga bao pekee na kuzima kelele za mashabiki wa Rukwa.

Kocha wa Mkoa wa Pwani, Hamidu Mwichande alisema kuwa ushindi huo unampa hamasa na morari ya kufikia lengo lake la kutwaa ubingwa.

Kocha wa timu ya Mkoa Rukwa, Lusekero Soud alisema wamepoteza mchezo kutokana na makosa madogo madogo waliyoyafanya vijana wake, lakini sasa wanatazama mechi zinazofuata.

Advertisement