Ndalichako awatega walimu
Muktasari:
Aliyasema hayo jana alipokuwa akizungumza na walimu wanaofundisha darasa la kwanza hadi la nne ambao wanafundisha kusoma kuandika na kuhesabu (KKK) katika shule za msingi za wilaya za Handeni na Bumbuli.
Tanga. Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako amesikitikia kitendo cha wanafunzi wa Mkoa wa Tanga kushika nafasi za mwisho katika mitihani ya kitaifa ya kidato cha nne kwa kuwa kinawavunja nguvu wazazi wao.
Aliyasema hayo jana alipokuwa akizungumza na walimu wanaofundisha darasa la kwanza hadi la nne ambao wanafundisha kusoma kuandika na kuhesabu (KKK) katika shule za msingi za wilaya za Handeni na Bumbuli.
Walimu hao wako kwenye mafunzo ya kuwajengea uwezo.
Profesa Ndalichako alisema kuanzia mwaka huu, hataki kuona shule za mkoa huo zikiburuza mkia katika mitihani yote ya Taifa.