VIDEO:Ushauri wa Ulimwengu na maswali kuhusu utafiti wa Twaweza

Mwanahabari nguli Jenerali Ulimwengu 

Muktasari:

Ulimwengu alisema anafikiri kwa viongozi  wangesema hilo linashtusha na kujiuliza linatoka wapi. 

Dar es Salaam. Mwanahabari nguli Jenerali Ulimwengu alitoa ushauri jana Julai 5 kutokana na utafiti wa Twaweza alisema ujumbe lazima ufikishwe kwa viongozi kuhusu hali ya watu kuwa na hofu.

Alisema ni muhimu huo ujumbe ukafikishwa kwamba kuna hofu inatawala. “Maaskofu wameongea hivi karibuni. Hawa si wale maaskofu wa chini ya miti, hapana, bali ni wa kiutamaduni wenye uongozi toka Roma.”

Ulimwengu alisema anafikiri kwa viongozi  wangesema hilo linashtusha na kujiuliza linatoka wapi. “Serikali inapaswa kujenga utaratibu wa watu kutoa mawazo. Watu wapinge na kuuliza maswali kwa nini mnafanya hivyo ndiyo mnajenga utaratibu huo. Lakini siyo kuwatisha. Wale hamuwezi kuwatisha, wale siyo Chadema.”

“Kama watu hawajulikani wako wapi, Ben Saanane hajulikani yuko wapi, Azory hajulikani, Lissu bado yuko Ubelgiji. Siyo kwamba imefanywa na CCM hapana.”

“Watu hawa wanatekwa, hawa wanapigwa. Hatujasema nani anawapiga, lakini kama unaletewa ripoti kila baada ya miezi mitatu kwamba mtu kapigwa risasi au mtu kapotea, ningekuwa na wasiwasi sana. Leo nina wasiwasi na siyo kiongozi, fikiria ningekuwa mtawala ningekuwaje?